Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET), Dkt Aneth Komba leo tarehe 14/05/2024 amefanya ziara ya kikazi katika shule ya msingi Makumbusho ya jijini Dar es Salaam kwa ajili kujionea utekelejezaji wa Mtaala ulioboreshwa kwa ngazi ya elimu ya Awali na Msingi.

Akiwa katika shule hiyo, Dkt. Komba amepata nafasi ya kufanya mazungumzo na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Bw. Elimoo Mghase aliyeambata na baadhi ya walimu wa masomo mbalimbali.

Dkt. Komba amefurahia kutembelea katika shule hiyo na kufahamu masuala kadhaa hasa katika utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa na kujua namna walimu waliopata mafunzo wanavyotekeleza kazi yao kwa ufanisi.

“Nimepata nafasi ya kuzungumza na walimu kadhaa wanaofundisha katika shule hii ya Makumbusho, imenisaidia sana kusikia mwenyewe juu ya kazi ya ufundishaji inavyoendelea na pia namna walimu wanavyojituma katika kazi.” Amesema Dkt. Komba.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi Bw. Mghase ameishukuru Serikali kwa kufanya uboreshaji wa Mitaala ya elimu ambayo inaendana na karne ya ishirini na moja hasa katika matumizi yua TEHAMA.

“Kwa kweli hii Mitaala inaendana na hali halisi ya Dunia inavyokwenda hasa katika masuala ya teknolojia. ”Amesema Bw. Mghase.

Ameendelea kusisitiza kuwa, walimu wa shule hiyo nao wamepata mafunzo ya walimu kazini na yale ya utekelezaji wa Mtaala uliobreshwa kama walimu wengine nchini.








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...