Timu ya madaktari bingwa 30 waliowasili mkoani Njombe wameanza kutoa huduma katika hospitali za wilaya zote mkoani humo huku wito ukitolewa kwa wananchi kujitokeza kupata matibabu ili kupunguza ghalama kwa kufuata huduma hizo katika hospital kubwa nchini.

Michuzi blog imefika katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena na kushuhudia huduma zikiendelea ikiwemo mama mjamzito aliyefanyiwa upasuaji kwa usalama chini ya uangalizi wa madaktari hao ambapo Erenestina Mwipopo Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Watoto anasema tayari ameanza kuwahudumia watoto na baadhi ya aliowahudumia ni wenye magonjwa ya Moyo,Kuzaliwa kabla ya wakati pamoja na Changamoto nyingine.

"Hapa Njombe mjini tupo madaktari bingwa watano na tumegawanyika kwenye idara tofauti lakini hapa kwenye watoto wachanga tumeshaanza kuwahudumia pia na kuna mtoto mwenye changamoto ya Moyo anapatiwa huduma na upande wa akina mama tayari upasuaji umeanza"amesema Dkt.Erenestina Mwipopo

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena Dokta Ayub Mtulo amesema wateja wameendelea kujitokeza katika hospitali hiyo ambapo wengi wao wamekuwa wakifika kwa dakatari bingwa wa wanawake na uzazi "Wanaofika kwa wingi ni wateja wa daktari bingwa wa wanawake pamoja na uzazi pamoja na magonjwa ya ndani lakini pia daktari bingwa wa upasuaji amepata wateja"

Timu hiyo ya madaktari bingwa ni miongoni mwa madaktari bingwa katika mpango kabambe wa utoaji huduma za kibingwa kwenye hospitali 184 katika ngazi ya halmashauri zinazofanywa na madaktari bingwa wabobezi wa Dkt. Samia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...