Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Bodi ya nyama Tanzania (TMB) imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazotolewa na mfanyabiashara maarufu anayejiita Mr maguruwe kuhusu ufugaji wa nguruwe unaofanyika katika kitongiji cha Zamahelo kata ya Zanka Wilaya Bahi Mkoani Dodoma.

Bodi ya nyama imemsajili mfanyabiashara huyo kama mfugaji mdogo wa nguruwe na kwa mujibu wa kanuni za bodi hiyo mfugaji mdogo wa nguruwe anatakiwa kuwa na nguruwe wasiozidi 49

Kaimu Msajili Bodi ya nyama Tanzania John Chasama ameyazungumza hayo leo mara baada ya kutembelea eneo la shamba la nguruwe la mfanyabiashara huyo (Mr Maguruwe)

"Mr Maguruwe amekuwa akitoa taarifa kwa watanzania kuwa wawekeze kwenye shamba lake la nguruwe jambo hilo sio sawa kwa kuwa kundi la usajili ambao amesajili ni kundi la wafugaji wadogo ambalo lina ukomo idadi ya nguruwe wanaotakiwa wanaotakiwa kuwa shambani"

Chasama amesema kwa wadau wote wanaojisajili katika Bodi hiyo uhai wa usajili wao ni kipindi cha mwaka mmoja na baada ya hapo anaomba tena kuhuisha usajili
wake .

Aidha Chasama amesema wamekuwa wakiona taarifa mbalimbali za mdau huyo akipotosha baadhi ya vitu juu ya sifa za nguruwe ikiwemo kutaja nguruwe aliyenao ni wa aina ya kipekee, wanaa uzito mkubwa unaofikia kilo 1,400 na kuhusianisha ulaji wa nyama ya nguruwe hao na mabadiliko ya maumbile ya akina mama

"Upotoshaji huu unaofanyika unaharibu taswira ya tasinia ya nyama ambapo tayari imeanza kukua kwa kasi na kuongeza mchango wake katika pato la Taifa "

Kwa upande wake Afisa Mkaguzi toka Bodi ya nyama Alex Mkenda amesema katikae kufanyae ukaguzi katika mabada ya mfanyabiashara huyo wa nguruwe wamebaini kuwa madanda hayo bado yako katika hali mbaya hayana ubora na anatakiwa kuyaboresha na pia aongeze ulinzi wa kudhibiti magonjwa na kufuata taratibu nzuri za kutenganisha mifugo hiyo wakubwa na wadogo.

Naye Afisa mifugo/ Mkaguzi toka Bodi ya nyama Tanzania Kiboma John amesema wanamshauri mfanyabiashara huyo kudhibiti maginjwa na kuangalia wale wanyama wapya wanaoingia wanapaswa wawe na sehemu yao na wale wagonjwa pia wawe na sehemu yao kabla ya kuchanganywa na wanyama wengine

"Ki Msingi tunapaswa kudhibiti magonjwa kuanzia sehemu ya kuingilia na hapa hakuna sehemu ambayo unaweza kukanyaga ili kuondoa vimelea vya magonjwa mfano tuna ugonjwa wa homa ya nguruwe na hapae mazingira yalivyo ni rahisi hawa nguruwe kuadhirika wote kwa hiyo ki msingi anapaswa eneo hili Kuhakikisha ulinzi wa vimelea vya magonjwa unakuwae wa uhakika"- Kiboma John

Hata hivyo Bodi ya nyama Tanzania inatoa rai kwa wadau wote ambao wamesajiliwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na maadili yanayosimamia sekta husika na kuitaka jamii Kwa ujumla kujiridhisha na taarifa zinazotolewa na wadau/wafanyabiashara kwa kuwasiliana na mamlaka husika.
Kaimu msajili Bodi ya Yyama Tanzania (TMB) John Chasama akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo Bodi hiyo ilipotembelea shamba la mfanyabiashara maarufu anayejiita Mr Maguruwe Bahi, Mkoani Dodoma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...