Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri wa Mkuu Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Mhe Deo Ndejembi amewaomba Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanawapa Ushirikiano Vijana wa TK Movement wawapo katika majukumu ya kuangazia fursa mbalimbali ili kujikomboa na changamotoya ajira inayowakabili.

Ndejembi ameyasema hayo mapema Leo hii May 25,2024 Jijini Dodoma wakati akitoa Hotuba yake kwenye Kongamano la Uzinduzi wa Mtandao wa Vijana Nchini ujulikanao kama TK Movement uliojumuisha Vijana mbalimbali kutoka Bara na Visiwani.

"Kwa sababu hiyo, sioni sababu ya kukataa ombi lenu la kupatiwa ushirikiano na viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali mnapofanya ziara kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwahamashisha na kuwaelimisha vijana wenzenu".

"Hivyo, Kwa niaba ya Waziri Mkuu, niwaombe Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji, Taasisi na Asasi mbalimbali muwape vijana hawa wa TK Movement ushirikiano wa kutosha wanapopita katika maeneo yenu kukutana na vijana wenzao kubadirishana mawazo na kuwapa mafunzo ya namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao huku wakiendelea kuyazungumzia mema na mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya sita".

Sambamba na hayo pia Waziri Ndejembi amewataka vijana hao wa TK kwenda kutoa elimu kwa vijana wengine juu ya kutojihusisha na mambo yasiyofaa ikiwemo Uvutaji wa bangi, matumizi ya dawa za kulevya,mapenzi ya jinsia moja kwani hayo ni moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakichangia Vijana kutoaminika jamii.

"Kwa kuwa mmeonyesha nia thabiti ya kuisaidia Serikali katika kushughulikia changamoto zinazowakabili vijana na wanawake, basi msiishie kwenye masuala ya uchumi peke yake. Nendeni mkawaase vijana wenzenu kujiepusha na tabia zinazopelekea mmomonyoko wa maadili kama vile ulevi wa pombe, uasherati, wizi, Mapenzi ya jinsia moja, uzururaji, matumizi ya dawa za kulevya nk. Hizi ni tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimewafanya vijana wengi wasiaminike na hivyo kukosa fursa mbalimbali kutokana na tabia hizo".

Awali akisoma Risala ya TK Movement Miss Alice Namara Erasto ambaye ni Mratibu Mkuu Msaidizi TK Taifa amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Mtandao huu hapa Nchini ni pamoja na kutambua nguvu ya kijana katika kuchangia uchumi wa nchi,kuzifikia ndoto na kukabiliana na vikwazo katika kuzifikia fursa zilizopo.

"Ndugu Mgeni rasmi,sababu zilizopelekea tuanzishe huu,mosi ni kutaka kutambua nafasi yetu kama nguvu kazi ya taifa katika kuchangia uchumi wa nchi yetu,pili kutambua fursa zilizopo katika kuzifikia ndoto zetu na tatu kukabiliana na vikwazo vinanvyotuzuia kuzitumia fursa zilizopo katika kufikia ndoto zetu".

"Mhe Mgeni Rasmi,ndoto yetu sisi vijana na wananwake wa Tanzania nj kuwa na kesho iliyo bora kuliko leo. Na huu ndio msingi wa jina la Mtandao wetu wa Taifa letu, Kesho yetu".

"Ndugu Mgeni Rasmi, kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Idadi ya vihanq wenye umri katika miaka 15-35 ni 21,312,411. Kati ya idadi hiyo wanaoishi vijijini ni 12,647,509 (59.3%) na wanaoishi mjini ni 8,664,902sawa na asilimia (40.7)".

Naye Naibu Waziri wa Michezo Hamisi Mwinjuma akitoa salamu zake amewatia moyo vijana kwa kuwaambia kuwa wasijali katika njia au mapito waliyoyapitia badala yale waamini kuwa kitu ambacho Mungua ameandaa kwaajili yao.

"Haijalishi unapitia nini au upo katika mapito gani katika yote amini pia jua iko njia Mungu ameweka ili wewe kufika katika kile alichokuandalia".

Naye Mhe Mariamu Ditopile mbunge wa viti Maalum Dodoma katika moja ya midahalo iliyokuwa ikiendelea kwenye mkutano huu amewataka vijana kuaamini na kutambua kuwa hakuna nyakati zinazodumu katika maisha hasa nyakati ngumu na kuwataka wajitume na wasibweteke.

"Nataka vijana waamini kuwa hakuna nyakati zinazodumu maishani hasa nyakati ngumu,lakini wajitume na wasibweteke na nafasi walizona na pia tuondoe unyonge".

Mbunge wa Buchosa naye Eeick Shigongo amewataka vija a kuwa na kiu na kuwa bora,kufanya kazi kwa bidii na kuwa nidhamu ya fedha.

"Vijana tujitahidi kuwa na kiu ya kuwa bora,kufanya kazi kwa bidii,kuwa na nidhamu ya fedha lakini pia kutosikiliza maneno kutoka wengine ya kukatisha tamaa badala yake isikiloze sauti iliyoko ndani yako".

Mkutano huu wa Vijana wa TK Movement uliozinduliwa leo Jijini Dodoma umehudhuriwa na Vijana takribani 1,330, kutoka Bara na Visiwani, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wahadhili wa Vyuo mbalimbali,Naibu Waziri wa Michezo na Viongozi wa Vijana kutoka vyama vya Siasa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...