Mapendekezo ya ripoti ya mageuzi ya sekta ya Elimu,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar inaendelea ikiwa ni kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu katika ngazi zote za elimu zikiwemo Skuli, Wilaya, Mkoa na Wizara.

Hayo ameseyasema Waziri wa Elimu Zanzibar Mhe.LelaMuhamed Mussa wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo katika Baraza la Wakilishi Zanzibar.

Amesema Kuimarisha mfumo wa tathmini ya maendeleo ya elimu ya wanafunzi katika ngazi zote za elimu na kupandisha ufaulu wao kuimarisha miundonmbinu ya Elimu

Aidha amesema katika kujenga madarasa 1500 kupitia ujenzi wa Skuli za Ghorofa, Skuli za Chini na kukamilisha madarasa yaliyoanzishwa na
wananchi, kwa Unguja na Pemba, nyumba 20 za walimu, Ofisi ya Wizara, Ofisi 4 za Elimu Wilaya, vyoo 300, Dakhalia 8 zikiwemo dakhalia za wanaume za Chwaka Tumbe na Paje Mtule pamoja na kuzifanyia ukarabati mkubwa na mdogo skuli 100 za Msingi na Sekondari. Kujenga karakana (workshop) za Elimu ya Amali

Hata hivyo amesema katika skuli 33 za Sekondari Unguja na Pemba (karakana 3 kwa kila Wilaya) na kujenga uzio katika skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame na Mohamed Juma Pindua.

Amesema kuimarisha matumizi ya tekonolojia katika kufundishia na kujifunzia kwa kuziunganisha na mkonga wa taifa taaasi za Elimu zikiwemo; skuli 217 za Sekondari, Vituo vya walimu 12 na Vituo vya Ubunifu wa Kisayansi (Hubs) 22 pamoja na kuzipatia vifaa vya TEHAMA.

Waziri huyo amesema katika kuendelea kutekeleza mtaala mpya wa umahiri kwakuwapatia walimu mafunzo na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vikiwemo vya Watoto wenye mahitaji maalumu. Kuimarisha Mafunzo ya Ufundi na Amali kwa vyuo vitano vya Mafunzo ya Amali, utanuzi wa Chuo cha Karume (KIST) na ujenzi wa chuo cha ubaharia na kuzipatia vifaa.

Waziri huyo amesema fursa ya upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar kuanzia ngazi ya Diploma pamojakuanza mradi wa kujenga kampasi ya kudumu ya Chuo cha IIT Madrasa; Ujenzi wa Jengo la Skuli ya kilimo, Jengo la maabara ya sayansi ya kisasa - SUZA, Ujenzi wa skuli ya Afya, skuli ya meno na kliniki yake -SUZA.

Amesema kuuimarisha huduma za maktaba kwa kuanza kujenga na kuimarisha maktaba mpya ya kisasa pamoja na maktaba mtandao (e-library)
 

Waziri wa Elimu  Zanzibar  Leila Mohamed  Mussa akiwasilisha  Bajeti ya Wizara ya Elimu Zanzibar katika Baraza la Wakilishi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...