Washindi wawili wa promosheni ya Twenzetu Dubai na Parimatch inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch wamepatikana na watasafiri Dubai Jumatatu ijayo.
Washindi hao ni Daniel Kasanga, mkazi wa Ruvuma na Mohamed Salim mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Parimatch, Ismail Mohamed.
Ismail
alisema kuwa Kasanga ni mshindi wa droo ya wiki ya kwanza na Salim
ameshinda droo ya wiki ya pili kupitia mchezo Aviator ndani ya Casino.
Alisema
kuwa safari hiyo itagharimiwa na kampuni yao ikiwa pamoja na usafiri,
visa, malazi kwenye hoteli ya kifahari na gharama za kutembelea maeneo
mbalimbali ya kitalii na kihistoria wakiwa Dubai.
“Kasanga
na Salim wameshinda tiketi ya Dubai kupitia mchezo wa Aviator ambao
unapatikana kwenye Casino ya Parimatch. Bado kuna nafasi za kushinda
safari ya kwenda Dubai pamoja na fedha taslim Sh200,000 kila siku ambazo
zinatolewa katika droo ya siku husika.
Tunawaomba wadau wetu kuendelea kubashiri na Parimatch ili kuweza kushinda zawadi hizo,” alisema Mohamed.Kwa upande wake, Kasanga alisema kuwa amefarijika sana kushinda safari hiyo ya kihistoria kwake.
“Pamoja
na kuwa na pasi ya kusafiria, sikujua lini nitaitumia pasi hiyo, hivyo
kupitia droo ya Twenzetu Dubai na Parimatch, ndoto yangu imefanikiwa,”
alisema Kasanga.Alisema kuwa amefarijika kushinda safari hiyo na pia
fedha taslimu Sh500,000 ambazo alizipata chapchap.Naye Salim alisema
kuwa hakuamini mara alipopigiwa simu kuwa ameshinda safari ya Dubai
kupitia promosheni ya Parimatch.
“Sikuamini,
kwani unawezaje kwenda kutembelea nchi ya kifahari, yenye raha na
vivutio mbalimbali kama Dubai kirahisi rahisi tu. Hata hivyo, kupitia
aviator, jambo hili limewezekan, nawaambia Watanzania wenye umri kuanzia
miaka 18, kubashiri na Parimatch, hawana longolongo,” alisema Salim.
Kampuni
ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa
ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya Ukaribisho ya 125% hadi kufikia TZs
1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao!
Parimatch imekuwa
ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri
ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua
kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya
Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira
wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na
pre-match.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya Parimatch, Eric Gelard (kushoto) akikabidhi ticket kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Twenzetu Dubai, Daniel Kasanga.
Balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Masatu Amos Ndalo (kulia) akizungumza na mshindi wa kwanza wa promosheni ya Twenzetu Dubai mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Masatu Amos Ndalo (kushoto) akizungumza na mshindi wa kwanza wa promosheni ya Twenzetu Dubai mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...