Na Janeth Raphael MichuziTv - KITETO, MANYARA

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye (mb) amewataka Wananchi wa kijiji cha Kinua kilichopo kata ya Namelock Wilayani Kiteto kutumia mtandao vizuri kwa kufanya mambo ya maana na sio kumtukana mtu au kuandika mambo yasiyofaa katika mitandao hiyo ikiwemo udhalilishaji wa Mitandaoni.

Waziri Nape ameyasema hayo mapema Leo hii May 13,2024 Mkoani Manyara katika Kijiji cha Kinua kilichopo Kata ya Namelock-Kiteto alipofanya Ziara ya kukagua upatikanaji wa huduma ya mawasiliano ya simu kwenye Mnara uliojengwa na Kampuni ya Aritel Tanzania chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Nakuongeza kuwa wao watapambana kuhakikisha mtandaoni pako salama lakini wananchi wahakikishe wanafuata taratibu na kutotumia mtandao hui vibaya.

"Sasa huko kwenye mtandao kwasababu kila mtu anaenda huku na hela zetu tunaweka huko,wote tunatembea huko na matapeli wapo huko. Sisi tutaoambana kuhakikisha pako salama lakini na ninyi hakikisheni mnafuata utaratibu msitumir mtandao vibaya ,usitumie kumtukana mtu, usijidanganye hata kwa kupiga picha za hovyo hala ukafuta jua kuwa utafuta kwako tu sisi tukitaka kuzipata tutazipata tu,tutumie vizuri yapo mambo mengi ya maana ambayo mnaweza kuyafanya msifanye mambo ya hovyo ukadhani utakimbia tutakukamata tu".

Mbali na hilo pia Waziri ametumia nafasi hii kuupongeza mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF kwa kuhakikisha wanasimamia vema dhamana waliyopewa ili kuleta mvuto wa kibiashara katika maeneo mbalimbali ambayo makampuni mengine ya mawasiliano ya simu hawakuweza kuyafikia.

"Nataka niupongeze mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) hawa wamepewa dhamana ya kuhakikisha kule kote ambako makampuni ya simu wasingeweza kupeleka Minara kwasababu kibiashara isingelipa, Serikali ya CCM ikaanzisha mfuko huu ili kule ambako mvuto wa kibiashara sio mkubwa sana mfuko utoe hela ili usaidie ujenzi wa Mnara kwani mnara mmoja ule ni karibia Milioni 350 kwa hali ya kawaida sio rahisi kujenga ila mfuko unasaidia. Mimj najisikia fahari kuwa Waziri ninayesimamia mfuko huu".

Naye Bwana John Mkondya ambaye ni Kaimu Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) amesema kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha wananchi walio wengi hapa Nchini hususan kata ya Namelock wanapata huduma ya mawasiliano ili kuboresha maisha na uchumj kwa ujumla.

"Lengo letu ni kuhakikisha wananchi walio wengi katika nchi hii hususan katika kata ya namelock Wilaya ya Kiteto wanaendelea kupata mawasiliano katika kuboresha maisha yao kijamii na kiuchumi".

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mhe Ole Lekaita amesema kuwa wao wanapata mianara mingi ya upendeleo lakini na minara bado wamepata miradi mingi yenye thamani ya milioni 25 ikiwemo chuo cha Veta,Shule za Sekondari na Vituo vya afya vote vikiwa ni vipya.

"Sisi tunaongoza mikoa mingi kwa kupata Minara mingi sana ya upendeleo na wilaya yetu ni kubwa. Lakini sio minara tu kwa miaka mitatu ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan tumepata miradi ya zaidi ya Shilingi milioni 25,tumepata Veta ambayo hapo awalj hatukuwa nayo,shule 4 za Sekondari mpya,Vituo 2 vya afya vipya na magari ya kubebea wagonjwa ma 3 na shule zingine za Sekondari 2 mpya pia hiyo ni kwa miaka 3 tu tofauti na hapo awali maendeleo kama haya tuliyapata kwa miaka mingi".

Akitoa salamu zake katika Mkutano huu Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Hadija Taya au maarufu kama Keisha ameiomba Jamii ya Kimaasai na wakazi wote wa Wilaya ya Kiteto kuwatia moyo na kuwaruhusu wanawake kushiriki katika kugombea nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa kwanj tayari tunao mfano mzuri wa namna ya uongozi kutoka kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Niwaombe jamii ya Kimaasai na wana Kiteto kwa ujumla muwaruhusu wanawake wa hapa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani Raisi Samia Suluhu Hassan ameshaonesha njia ya jinsi ya kufanya katika uongozi".

Mnara huu uliokaguliwa leo na Waziri Nape umegharimu kati ya milioni 300 mpaka milioni 350 na ni moja kati ya Minara 758, Ujenzi wake unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...