AIRTEL TANZANIA leo Juni 11, 2024 imekabidhi hundi ya TZS 40,842,742,033.15 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni malipo ya gawio la mwaka wa fedha 2023/24. Gawio la Airtel kwa serikali limewasilishwa leo katika hafla maalum ya Siku ya Gawio la Mwaka 2024 iliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Ikulu jijini Dar es salaam. Hafla ya hiyo makabidhiano ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kupitia hafla ya Kugawa Gawio kwa serikali Airtel Tanzania ni miongoni mwa kampuni za biashara tatu zilitoa kiasi kikubwa cha Gawio mwaka huu kati ya kampuni za biashara ambazo serikali ina hisa ndani yake kwa mwaka huu. Tangu mwaka 2019, Airtel Tanzania Plc na Airtel Money Tanzania Limited zimekuwa zikitoa Gawio kwa Serikali ikiwa ni matokeo ya jitihada za Airtel katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa. Serikali inaumiliki wa hisa asilimia 49 ndani ya Airtel Tanzania, ambapo kutokana na utaratibu huu wake wa kutoa Gawio kwa serikali tayari Airtel imelipa gawio la zaidi ya TZS 200 bilioni, na hivyo kudhihirisha nafasi ya ubia wake kama mshirika anayechochea maendeleo nchini wa Tanzania.

Akizungumzia hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na wadau wa sekta mbalimbali za maendeleo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Eliud Sanga alieleza kuwa Airtel Tanzania inawekeza katika ukuaji wa taifa kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika teknolojia na mawasiliano.

“Mikakati madhubuti ya serikali katika kushughulikia changamoto za uwekezaji na sera Madhubuti zimejenga mazingira bora hata kwentu Airtel katika kustawisha bishara na kukabiliana na soko la ushindani, kwa hilo tunatoa shukrani zetu” alisema.

Sanga aliongeza kuwa, Airtel inafanya kazi bega kwa bega na serikali katika kusambaza bidhaa na huduma kwa gharama nafuu na kulingana na mahitaji ya wateja . Pia alizungumzia mradi waliozindua hivi karibuni wa Airtel Tanzania katika kuendeleza ajenda ya serikali ya elimu ya kidijitali. “Mfano mzuri ni mradi wa Airtel kinara wa ‘Airtel SMARTWASOMI’ uliozinduliwa hivi karibuni na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa msaada wa UNICEF na Wizara ya Elimu na Wizara ya Serikali za Mitaa”.

“Airtel SMARTWASOMI imezinganisha na mtandao wa Intaneti shule 50 za sekondari zilizopo Zanzibar, Dodoma, na Mbeya kuwa madarasa mahiri, na kunufaisha zaidi ya wanafunzi 55,000 na kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya 2,000. Miradi kama hii inadhhirisha dhamira yetu ya kutumia teknolojia kwa maendeleo bora ya elimu na kukamilisha mpango wa serikali katika kutoa elimu bila malipo kwa kila mtoto”, alisema Sanga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh alieleza kuwa gawio iliyowasilishwa mbele ya Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan inadhihirisha dhamira ya kampuni Airtel katika ustawi wa uchumi wa Tanzania. Balsingh alisisitiza umuhimu wa kuongeza matumizi na uwepo wa simu za janja ili kuongeza kasi vijana kutumia huduma za data na huduma za kifedha kwa maendeleo yan chi.

“Ahadi yetu kama Airtel Tanzania ni kutoa huduma za mawasiliano kwa urahisi na kwa gharama nafuu. Tunazidi kujionea jinsi gani ongezeko la matumizi ya simu janja zinavyochangia na kuchochoea upatikanaji wa taarifa kwa vijana na huduma za kifedha,” alieleza Balsingh.

Balsingh aliongeza zaidi “Idadi ya watumiaji wa simu nchini Tanzania imeongezeka kwa kiasi kikubwa, Hii ni kufatia ripoti ya GSMA, ambapo asilimia 72 ya Watanzania wanatumia huduma za fedha kwa njia ya simu, na hivyo teknolojia inaendelea kutoa masuluhisho mbalimbali ikiwemo hii ya kupanua upatikanaji wa fedha nchini.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...