Na Mwandishi Wetu

Wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu Zanzibar wameipongeza kampuni ya Barrick nchini na wadau mbalimbali kwa kudhamini kongamano la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ili ya kuwajengea uwezo wa kujimini na kutambua fursa mbalimbali za kimaisha.

Kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka, limeandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania)

Wakiongea kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki wakati wa kongamano la hilo, lililofanyika Zanzibar baadhi ya wanafunzi walisema wameweza kujifunza mengi kupitia kongamano hilo sambamba na kujua shughuli za taasisi mbalimbali kubwa nchini na jinsi ya kutafuta fursa za ajira kwenye taasisi hizo ikiwemo jinsi ya kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao.

“Makongamano kama haya ni moja ya njia ya kujifunza kwa kuwa kuna mambp mengi yanaendelea wanafunzi tunakuwa hatuyafahamu zaidi ya kufuatilia masomo anayofundishwa darasani “alisema Ally Salum Khamisi,Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar.

Kupitia kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.

Maofisa Raslimali Watu Waandamizi wa Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na waadhiri kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo viongozi wanaosimamia sekta ya elimu Zanzibar na mgeni rasmi alikuwa ni Meya wa manispaa ya mjini magharibi Mh.Haji Ali Haji.

Rais wa  Serikali ya  Wanafunzi wa SUZAKO, Khalifa Juma Ameir
 akizungumza Katika Kongamano la  wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ili ya kuwajengea uwezo wa kujiamini na kutambua fursa mbalimbali za kimaisha.

 Kongamano hilo lililofanyikia Zanzibar, liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania).
 

Timu ya wafanyakazi wa Barrick na Wanafunzi  kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya Juu wakiwa katika kongamano hilo



 

Mwakilishi wa AIESEC akiongea katika kongamano  hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...