BENKI ya Exim Tanzania imezindua kampeni maalum inayolenga kuwashawishi wateja wake wanaomiliki simu za mkononi kufanya miamala zaidi kwa kutumia simu zao pamoja na kutumia mtandao badala ya malipo ya fedha taslimu pindi wanapohitaji kutumia huduma mbalimbali za kibenki. Kampeni hii ya miezi mitatu itaambatana na zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kila wiki na mwezi kwa washindi.

Kampeni hiyo iliyopewa jina la 'Tap Tap Utoboe' inatoa fursa kwa zaidi ya washindi 200 miongoni mwa wateja wa benki hiyo wanaotumia simu zao au mtandao kufanya miamala, kuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, pikipiki, bajaji pamoja na zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Mazda CX-5.

Tap Tap Utoboe inalenga wateja wa sasa na wateja wapya. Kwa mteja ambaye hajawahi kutumia huduma za kibenki za simu za mkononi na mtandaoni, hii ni fursa yake kujiunga. Kwa wateja wapya, waalikwa kujiunga na familia ya Exim Bank na kufurahia huduma zao bora za kibenki za kidigitali. Ili kushiriki, mteja anatakiwa kufanya miamala yake yote ya kibenki kupitia simu yake au mtandao, ikiwamo kulipia ankara za maji, umeme au visimbusi vya television, malipo ya manunuzi, kutuma pesa, kulipia kodi,, kutoa fedha kwa Exim Wakala, kulipia bima ya vyombo vya moto, na huduma nyenginezo.

Ili kushinda zawadi, mteja anahimizwa kufanya miamala ya mara kwa mara kupitia huduma za kibenki za simu za mkononi na mtandaoni. Washindi kumi wa kila wiki watapata TZS 50,000 kila mmoja, na washindi kumi wa kila mwezi watapata TZS 100,000 kila mmoja. Mshindi wa tatu atapata pikipiki, mshindi wa pili atapata bajaji, na mshindi wa kwanza na jumla ataondoka na gari mpya kabisa aina ya Mazda CX-5.

Kwa mujibu wa Exim Bank wakati wa kampeni hiyo kila muamala wenye thamani ya Tsh 50,000/= na zaidi ukiwa umefanyika kwa zaidi ya mara moja kupitia simu ya mkononi au mtandao, muhusika atastahili kushiriki bahati nasibu ya kumpatia mshindi.

“Kila wiki, kutakuwa na droo na wateja 10 watakaobahatika watapata nafasi ya kujishindia zawadi ya fedha taslimu TZS. 50,000/=.’’ Alitaja, huku akiongeza: “Aidha, kila mwezi kutakuwa na droo ambapo wateja 10 watapata nafasi ya kujishindia fedha taslimu TZS 100,000 huku sifa ya chini katika droo hii ya mwezi ikiwa ni mhusika kufanya miamala yenye thamani ya TZS 200,000 na zaidi katika huduma moja au zaidi.''

Huduma za kibenki za simu na mtandaoni za Exim Bank zimeundwa kurahisisha maisha ya mteja kwa kuhakikisha upatikanaji, urahisi, na usalama wa miamala yake. "Tunataka wateja wetu wafurahie urahisi na manufaa ya huduma za kidigitali huku wakiwa salama na kufurahia ufanisi wa miamala yao," alisema Lyimo.

Silas Matoi, Mkuu wa Njia Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali, alisema, "Ubunifu wa kidijitali ni msingi wa mkakati wetu. Kampeni ya Tap Tap Utoboe imeundwa kuhusisha watumiaji wa teknolojia na wale wasioijua sana, kuhakikisha kila mmoja anafaidika na huduma zetu."

Akizungumzia zawadi kuu kwa washindi wa kampeni hiyo, Silas alisema “Hivyo basi mshindi wa kwanza atajishindia zawadi ya gari mpya kabisa aina ya Mazda CX-5 ambayo iko tayari kuingia barabarani, iliyokatiwa bima kubwa (comprehensive). Mshindi wa pili yeye ataondoka na Bajaj na mshindi wa tatu atajipatia pikipiki”.

“Tunajivunia ushirikiano wetu na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania katika kampeni hii. Ushirikiano huu ni endelevu na unalenga kuhakikisha kampeni hii inafanyika kwa ubora na ufanisi mkubwa” aliongeza.

Kupitia kampeni hii ya 'Tap Tap Utoboe', Exim Bank inalenga kukuza uchumi jumuishi kwa kuwapa wateja fursa sawa za kupata huduma za kifedha. Huduma za kibenki za simu na mtandaoni za Exim Bank zinatoa fursa kwa watu wote, wakiwemo wale wa vijijini, kupata huduma za kibenki kwa urahisi zaidi. Hii inasaidia kuongeza ushirikishwaji wa kifedha na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu alisema dhamira ya msingi ya benki hiyo ni kuandaa jamii yenye utamaduni wa kutotembea na pesa taslimu na badala yake wafanye miamala kwa njia za kielectroniki hatua ambayo pia imekuwa ikipigiwa chapuo na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia katika kufanya miamala ya kifedha.

“Benki yetu kihistoria imekuwa mstari wa mbele kuleta mageuzi ya kihuduma hapa nchini. Katika kufanikisha mageuzi hayo tumekuwa tukitumia namna mbambali ikiwemo kutoa zawadi kwa wateja wetu ili tu tuweze kwenda nao sambamba katika mageuzi haya. 

Tunaamini kupitia kampeni hii tunakwenda kuleta mabadiliko yenye tija na faida kubwa kwenye mfumo mzima wa sekta ya fedha hapa nchini na iatawapa wateja wetu fursa ya kufurahia huduma za kibenki zenye urahisi wa matumizi, upatikanaji wa haraka, na uaminifu. Hii ni sehemu ya kujitolea kwetu katika kuboresha huduma kwa wateja wetu na kuwahamasisha kutumia huduma zetu za kidijitali’’ alisema.

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu (kulia), akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani), kuhusu kampeni ya ‘Tap Tap Utoboe’ inayohimiza wateja kufanya miamala zaidi kwa kutumia simu za mkononi na majukwaa ya mtandaoni badala ya malipo ya pesa taslimu. Tukio hilo lilifanyika katika makao makuu ya benki hiyo tarehe 10 Juni, 2024. Wateja watapata nafasi ya kushinda fedha taslimu kila wiki na mwezi, pikipiki, bajaj, na mshindi wa kwanza atashinda gari mpya aina ya Mazda CX-5. Katikati ni Balozi wa Kampeni hiyo, Idris Sultan akiwa na Mkuu wa Njia Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali wa Exim Bank Silas Matoi.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...