NA WILIUM PAUL, MOSHI.

CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro kimewaonya baadhi ya Wanachama wa chama hicho ambao wamegeuka kuwa vishoka wa siasa na kuanza kupita hovyo na kuwafanya viongozi waliopo kushindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi kuacha mara moja.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alipokuwa akifunga kambi ya siku tano ya vijana 300 wa chama hicho manispaa ya Moshi katika kata ya Kibosho wilayani Moshi.

Alisema kuwa, Wabunge na Madiwani waliopo madarakani kwa sasa wanatokana na CCM ambapo hutekeleza Ilani ya CCM na kuwataka wanachama kuwaunga mkono na pindi muda utakapofika ndipo kila mmoja ataruhusiwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali.

“Wapo watu wameshaamuwa kuwa vishoka wa siasa kwa sasa wanazurura na kuwafanya wale waliobeba bendera ya ccm badala ya kufanya kazi yao kuanza kupambana nao tambueni hawa hawafanyii kazi Ilani nyingine bali hufanyia kazi Ilani ya CCM na kipimo chao kinatokana na utekelezaji wa Ilani tuwaache watekeleze wajibu wao” alisema Boisafi.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa, kama yupo Diwani au Mbunge alisiyetekeleza majukumu yake aitwe kwa mujibu wa vikao vya kamati usika na kupewa maelekezo ya nini afanye ikibidi kupewa onyo ili kuhakikisha Ilani inatekelezeka.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi manispaa ya Moshi, Sadath Ndibalema aliiomba ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Serikali znapojitokeza fursa za vijana waweze kutumia vijana hao waliohitimu katika kambi hiyo kwani wamejifunza uzalendo, ujasiria mali na utiii.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro, Ivan Moshi alisema kuwa, watu ambao watakifanya chama kishinda kwa urahisi katika uchaguzi mkuu wa 2025 ni viongozi wa dola waliochaguliwa mwaka 2020.

Alisema kuwa, baadhi ya Madiwani wamekuwa hawafanyi mikutano ya hadhara ya Wananchi lakini wamekuwa wakisuguana na Wabunge ambapo kila mmoja amekuwa akimtupia lawama mwenzake na kukiomba chama kuhakikisha kila kiongozi anatimiza wajibu wake.

Naye Mkuu wa wilaya ya Moshi, Zephania Sumaye alisema kuwa, chama cha Mapinduzi kinahitaji vijana jeuri na wenye akili ya kuhoji jambo na kuweza kulitetea mbele ya jamii.

Sumaye alisema kuwa, kesho ya Tanzania imewekwa katika mabega ya Vijana na sio rasilimali zilizopo ambapo kambi hizo zinasaidia vijana kupata elimu na kuwavija na vijana wenye uwezo wa kuhoji na kutambua mambo mbalimbali ya chama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...