Katibu Mkuu wa  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Komredi. Jokate Mwegelo, amepokelewa na maelfu ya Vijana wa mkoa wa Iringa kwa nyomi ya aina yake wakiwa na sura zenye kuleta tafsiri ya furaha za mioyo yao.


Akipokelewa katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi katika mapokezi yaliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara Komredi. Mussa Mwakitinya, maelfu ya vijana wametanguliza salamu zao za shukrani kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kutekeleza majukumu yake ndani ya Chama na Nchi kwa ujumla huku wakimtaka Katibu Mkuu Jokate kufikisha salamu zao hizo.


Komredi Jokate amewasili mkoani Iringa kwa mapokezi, kutembelea chuo cha Ihemi na kukagua shughuli za chuoni hapo pamoja na Kukagua eneo la Igimbilo lenye ukubwa wa ekari 80.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...