Katibu  wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ally Bananga  akizungumza  kwenye maadhimisho  ya miaka miwili  ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Kupinga vitendo vya rushwa ACVF iliyofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam


Kaimu Afisa Usalama Barabarani (RTO) Kinondoni  ASP Notker Kilewa  akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo amekemea utoaji na upokeaji wa rushwa kwa raia



Kamanda TAKUKURU wa Ubungo  Devota Mihayo akizindua  mfumo mpya na wa kisasa wa kusajili mabalozi wa kupinga rushwa



Na Khadija Kalili, Michuzi Tv

KATIBU wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es salaam Ally Bananga amezitaka Asasi za Kiraia zilizo katika Mkoa huo katika utendaji wa shughuli zao za kila siku katika jamii waongezee jukumu la kutoa elimu ya kupinga vitendo vya rushwa katika jamii inayowazunguka hususani katika kipindi hiki kuelekea chaguzi za serikali za mitaa zitakazo fanyika baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

Muenezi Bananga amesema hayo huyo leo Juni 9 katika hafla ya sherehe ya maadhimisho ya miaka miwili ya programu ya badili tabia Sepesha Rushwa iliyoambatana na mahafali ya kwanza ya wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali ambao ni mabalozi wa Sauti wapinga rushwa Tanzania (ACVF AMBASSADORS) iliyofanyika Ubungo plaza Jijini Dar es salaam.

Amesema Asasi hizo zinaowajibu wa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupinga vitendo vya rushwa nchini kwa kuongeza hatua nyingine ya utendaji wa shughuli zao ikiwa ni pamoja na shughuli yao ya kujihusisha na kumpamba Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utendaji wake wa kazi wa kika siku.

" Ongezeni jukumu la kutoa elimu ya kupinga vitendo vya rushwa katika jamii inayowazunguka hii itasaidia wana jamii kuingiwa hofu ya kutoa na kupokea rushwa" amesema Bananga.

Aidha Bananga amesema kuwa Taasisi hiyo ya ACVF wao wamejipambanua kivyao kwa kupambana na rushwa na dhulma na kujitofautisha na Taasisi zingine ambazo zimekua zikifanya zikifanya machagizo kwa serikali na Rais wetu kwa zaidi kumpamba sasa waongeze hatua moja ya kutoa elimu ya kupinga vitendo vya rushwa.

Ameongeza kwa kusema kuwa

“Tunapoelekea katika chaguzi za serikali za mitaa Asasi za CHAMATA, WAMATA, Wazalendo huru na nyinginezo mnapo kwenda kwenye mitaa muende na ujumbe wa wazi kwamba rushwa ni adui wa haki yaani hata wale wanaokwenda kuchaguliwa wajue kwamba rushwa ni adui wa haki tangu wanaingia kuchaguliwa wajue kwamba hata sisi tunaowachagua tunapinga Rushwa” .

“Hata kwenye nguo( flana) mnazovaa pamoja na ujumbe za taasisi zenu lakini pia muweke na ujumbe wa kuonyesha mnapinga vitendo vya rushwa wazi wazi kwasababu najua kila mahali nyinyi mpo hivyo hakikisheni mnaisaidia nchi, jamii na mnaunga mkono jitihada za kupinga vitendo vya rushwa nchini”

Ameongeza kwa kusema kuwa malengo ya kuundwa kwa CCM katika katiba yake ibara ya tano msitari wa 16 inasema kuhusu kuona hakuna vitendo vya rushwa, uonevu, au upendeleo ambapo pia katika ahadi za wanachama ahadi namba nne inasema rushwa ni adui wa haki kwamba sitopokea wala kutoa rushwa ambapo pia katika kipengele cha uongozi kifungu cha 18 inasema kupokea mapato ya kificho au kupokea ama kutoa rushwa hiyo ni miiko ya kiongozi.

"Ukimuona kiongozi anafanya hayo hiyo ni tabia yake kwamba CCM kinakataa wazi wazi katika ahadi zake masuala ya rushwa na ndiyo maana TAKUKURU imeundwa na serikali ya CCM lakini hata mahakama ya mafisadi imeundwa na serikali ya CCM".

Kaimu Afisa Usalama Barabarani (RTO) Kinondoni ASP Notker Kilewa amekiri kwamba Jeshi la Polisi limekuwa likilalamikiwa kwa vitendo vya kutoa na kupokea rushwa lakini ameitaka jamii kutokuwa sababisho la kuchochea vitendo vya kutoa na kupokea rushwa kwa kuzingatia na kutii sheria za nchi.

Kamanda wa TAKUKURU Ubungo Devota Mihayo amesema kipindi cha chaguzi siyo kipindi cha wagombea na viongozi pekee bali ni kipindi cha wote maana kipindi hicho ndiyo kinatoa viongozi kwani ni kipindi ambacho wananchi hujiamulia nani awaongoze katika kipindi cha mika mitano inayokuja.

“Niwaombe msikubali kupokea chochote kwa kusema huyu ni mwenyekiti wa mtaa ndiye huwa katika ngazi ya karibu kabisa katika jamii na ndiyo hutumika kuwezesha kupatikana kwa Diwani, Mbunge na mustakabali wa maendeleo ya taifa kwa ujumla hivyo ni lazima tuanze kuipinga rushwa hapo”

“Hii elimu tukaitoe kwenye jamii kwakushirikiana na mabalozi wetu” amesema Kamanda wa TAKUKURU Ubungo ambaye ndiye alikua mgeni rasmi.

Awali Katibu Mtendaji Taifa wa ACVF Sauti Wapinga Rushwa Tanzania Kubega Dominiko amesema taasisi hiyo inampango wa kutoa elimu katika jamii kuhusu kupinga vitendo vya rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

"Changamoto ambazo tunakumbana nazo ni ukosefu wa ofisi zenye kukidhi mahitaji hasa katika ofisi zetu zilizopo Dodoma, Arusha na Dar esalaam tunayo nia ya kutanua wigo kwa kufungua ofisi katika mikoa mingine lakini hali imekua ngumu kutokana na kutegemea michango ya ada ada za mabalozi ambayo ni 1000 huku wengine wakishindwa kulipa licha ya udogo wa kiwango tulichokiweka

tunapenda kusema kuwa tunafanya kazi katika mazingira magumu hivyo tunaomba serikali iweze kuangalia namna ambayo inaweza kutukwamua,tulianza na mabalozi 50 na sasa wamefika zaidi ya 1500 na tuna imani idadi hii itaongezeka zaidi kwani vijana wengi wamekua na mwamko" amesema Katibu Mkuu huyo wa ACVF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...