Na MWANDISHI MAALUM-Lagos, NIGERIA

KATIKA kuhakikisha fursa za Tanzania zinatangazwa uptia diplomasia ya uchuni, Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, umeendesha jukwaa la kuvutia uwezaji nchini Nigeria.

Majukwaa hayo ambayo yamefanyika juzi na jana katika majimbo ya Enugu na Lagos kwa lengo la kjua mkakati wa uwekezaji nchini Tanzania ambapo ilizishirikisha makampuni yenye uwezo wa kuwekeza nje ya Nigeria.

Aidha, Ubalozi ulishirikiana na Kituo cha Uwekeaji Tanzania (TIC), na kuwakilishwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dkt. Binilith Mahenge na Afisa Uwekezaji Mwanadamizi wa TIC, Gaudence Mmassy.

Kutokana na umuhimu wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ubalozi uliratibu jukwaa hilo hilo na kuendelea kuwahimizi wawekezaji kuwekeza Tanzania kutokana na kuwa na mazingira wezeshi ya uwekezaji, maliasili mbalimbali na sheria na sera rafiki, amani na utulivu. 

Kutokana na Mkutano huo, kampuni zaidi ya 30 yameonesha utayari wa kuja nchini Tanzania kufanya ziara ya kibiashara na kupata taarifa zaidi kwa ajili ya kufanya maamuzi ya uwekezaji.

Makampuni hayo yapo katika sekta ya afya, utalii, ujenzi wa nyumba, viwanda, madini, mafuta, gesi asilia na Kilimo.

Ikumbukwe kwamba Nigeria ni nchi ya Pili kwa utajiri Barani Afrika na ina matajiri wengi wenye ukwasi na utayari wa kuwekeza nje ya mipaka ya Nigeria.

Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Binilith Mahenge akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wamiliki wa kampuni kubwa za nchini Nigeria ambao wameonyesha utayari wa kuja kuwekeza nchini. Na Mpigapicha Maalumu








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...