Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
CHUO cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinatarajia kufanya kongamano lake la 12 la Kisayansi litakalojadili tafiti mbalimbali hususan zile zenye majibu ya magonjwa yasiyoambukiza.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesemwa hayo leo Juni 24, 2024 wakati akizungumza na waandishiwa habari juu ya kongamano hilo la kisayansi litakalofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 27 na 28 mwaka huu katika Kituo cha Afrika Mashariki cha Umahiri wa magonjwa ya moyo, mishipa na Damu .

Amesema kongamano hilo linatarajiwa kuwa na wajumbe zaidi ya 400 kutoka ndani na nje ya nchi ambapo tafiti za kisayansi 80 zitawasilishwa kwa njia ya maongezi huku zingine 107 zitawasilishwa kwa njia ya mabango.

Amesema, jukumu la Muhas ni kutoa mafunzo ili kujenga rasilimali kwa watu wa fani ya afya , kufanya utafiti na kushiriki kikamilifu katika utoaji huduma ya afya katika jamii" amesema.

"Kongamano hili ni sehemu ya kumuenzi Mkuu wa chuo hiki wa kwanza aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Hayati Al Hassan Mwinyi pia limebeba kauli mbiu isemayo 'Sayani kama hadithi ya Maisha : nguvu ya tafiti, ubunifu na ushirikiano katika kuimarisha mifumo thabiti wa afya" amesema Profesa Kamuhabwa

Amesema kuwa katika kongamano hilo baadhi ya matokeo ya tafiti zitakazowasilishwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma wodi maalum za kulaza watoto wachanga ni asilimia 48, asilimia 15 ya wagonjwa wa VVU wana kiwango cha juu ya sukari unywaji wa pombo na shinikio la juu la damu lichangia wagonjwa hawa kuwa na kiwango cha juu cha sukari.

Amesema Tafiti nyingine ni ile iliyofanywa Kinondoni ambapo asilimia 54.5 ya wanawake wanaojichibua wengi wao wanoafanya kazi ya mapokezi.

Amesema kuwa kutakuwa mijadala mingi kuhusu ustawi wa afya ambapo kutakuwa na wataalam kutoka nje na ndani ya nchi.

Mijadala mingine itahusisha ufanisi wa kugaramia mifumo ya afya nchini( Health system financing ambapo watafiti watawasilisha jinsi gani nchi yetu itaweza kutekeleza mfumo huuu ili kuleta tija kwa wananchi wote.

Mifumo bora ya kuishi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza (health living and health aging)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...