Mratibu wa mama na mtoto mkoa wa Njombe Felisia Hyera ametoa wito kwa wazazi na walezi kutunza vizuri familia zao ikiwemo pia kuimarisha lishe ya familia pamoja na kusimamia makuzi ya watoto ili kuepusha mimba za utotoni ambazo pia zimekuwa zikisababisha mabinti wengi kuingia kwenye upasuaji hali inayopelekea kuwa na kizazi chenye ulemavu kwa kushindwa kufanya kazi.

Ametoa wito huo kwenye kikao cha utekelezaji wa programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM) unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la UWODO kwa kushirikiana na serikali ambapo amesema kitendo cha wanawake wengi kufanyiwa upasuaji ni hatari kubwa kwa kuwa taifa linazalisha walemavu kwa kushindwa kufanya kazi.

"Tunakutana na mabinti wengi wenye vidonda vya upasuaji na hii ni hatari kwasababu tukifanya upasuaji leo ujue ujauzito utakaofuata pia ni upasuaji kwa hiyo tunatengeneza vilema huko mtaani unakutana na binti mdogo anasema baridi inanisumbua ujue huyo shambani haendi na huwezi ukampa heka heka,hapo tunaharibu kizazi chetu kwa kuwa na vilema ambao hawafanyi kazi kama tunavyotarajia"amesema Felisia Hyera

Naye mkurugenzi wa shirika la UWODO bwana Hamis Kassapa ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanakuwa katika malezi,makuzi na tamaduni zetu ili kuondokana na adha mbalimbali ikiwemo ya kuua watoto pamoja na udumavu unaoendelea kutesa jamii hususani watu wa mkoa wa Njombe.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...