Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Fatma Toufiq amemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhimiza Nishati safi ya kupikia ikiwa ni agenda ya kumtua Mama kuni kichwani.

Hiyo ni miongoni mwa mkakati jumuishi wa kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili mpaka kufikia 2034 wananchi zaidi ya 80% wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi na mkaa ulioboreshwa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 200 kwa wanawake wajasiriamali,mama lishe wa Wilaya ya Mpwapwa Iliyotolewa kwa Ushirikiano wa Kampuni ya Oryx, Mbunge toufiq amewataka wanawake hao kutumia nishati ya gesi katika shughuli zao za ujasiriamali na kuepuka matumizi ya kuni.

"ule utaratibu wa kukimbizana na mikaa,kuni lakini sasa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anataka kumtua Mwanamke kuni kichwani badala yake aweze kutumia nishati safi na salama"

Aidha, ameahidi kuendelea na programu hiyo kwa wakinamama wa wilaya zote za Dodoma ili kuwatua kuni kichwani na kusaidia kulinda mazingira.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...