Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameungana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kutoa salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa familia ya Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa familia ya Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.

Balozi Mussa na Mhe. Kawawa wakimfariji Prof. Eliamani Sedoyoka ambaye ni mume wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi.Balozi Mussa na Mhe. Kawawa wakitoa faraja kwa wazazi wa marehemu.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipoungana na waombolezaji wengine katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...