Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika kikao chake cha 195 kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake CPA. Prof. Sylvia S. Temu imeidhinisha matokeo ya mitihani ya 99 ya Bodi kwa Watahiniwa waliofanya mitihani hiyo iliyofanyika mwezi Mei 2024 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi hiyo ya NBAA.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bodi ya NBAA, CPA. Pius A. Maneno amesema kuwa matokeo hayo yameidhinishwa kufuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 12 vilivyopo Tanzania Bara na Visiwani.

Amesema Jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 7,602 kati ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mitihani watahiniwa 642 sawa na asilimia 8.4 hawakuweza kufaya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali hivyo idadi ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo walikuwa 6,960 sawa na asilimia 91.6, kati ya hao watahiniwa 3,610 sawa na asilimia 51.9 walikuwa Wanawake na watahiniwa 3,350 sawa na asilimia 48.1 walikuwa Wanaume.

CPA. Maneno amesema jumla ya watahiniwa 394 wamefaulu mitihani ya Shahada ya Juu ya Uhasibu nchini yaani CPA (T). Kati ya watahiniwa hao wanawake ni 205 sawa na asilimia 52 na Wanaume ni 189 sawa na asilimia 48. Idadi hii inafanya jumla ya watahiniwa waliofaulu mitahani ya CPA kufikia 13,355 tangu mitihani hiyo ianze mwaka 1975.

Kati ya watahiniwa 394 waliofuzu kutunukiwa Cheti cha Taaluma ya juu ya Uhasibu wengi wao wametoka katika vyuo mbalimbali ambapo watahiniwa 88 sawa na asilimia 22.5 wametoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), watahiniwa 65 sawa na asilimia 16.5 wametoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), watahiniwa 59 sawa na asilimia 14.9 wametoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, watahiniwa 33 sawa na asilimia 8.4 wametoka Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) na watahiniwa 20 sawa a asilimia 5.1 wametoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Amesema jumla ya watahiniwa 10 wamefaulumitihani ya CPA(T) linganifu (Equivalent Qualification) kati ya hao wanawake ni 04 sawa na asilimia 40 na wanaume ni 06 sawa na asilimia 60 ambapo mpaka sasa jumla ya watahiniwa waliofaulu mitihani hii wamefikia 309 tangu mitihani hii ianze Novemba 2014.

Pia amesema katika ngazi ya awali ya Uandishi na Utunzaji wa Hesabu(ATEC I) watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 121 kati ya hao watahiniwa 09 sawa na asilimia 7.4 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 112 sawa na asilimia 92.6.

Pia ameeleza kuwa kati ya watahiniwa 112 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 89 ambao ni asilimia 79.5 wamefaulu mitihani yao na kati ya hao watahiniwa 33 sawa na asilimia 29.5 wanastahili kutunukiwa barua za ufaulu na watahiniwa 56 sawa na silimia 50 wamefaulu baadhi ya masomona watahiniwa 23 sawa na asilimia 20.5 hawakufaulu mitihani yao.

Aidha amesema katika hatua ya pili ya Cheti yaani ngazi ya uandishi na Utunzaji wa Hesabu(ATEC II) waliojisaliwa walikuwa 193 kati ya hao watahiniwa 16 sawa na asilimia 8.3 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 177 sawa na asilimia 91.7.

“Kati ya watahiniwa 177 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 151 ambao ni asilimia 85.3 wamefaulu mitihani yao ambapo kati ya hao watahiniwa 91 sawa na asilimia 51.4 wanastahili kutunukiwa Barua za Ufaulu na watahiniwa 60 sawa na asilimia 33.9 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii na watahiniwa 26 sawa na silimia 14.7 hawakufaulu mitihani yao” Alisema Maneno

Amesema katika ngazi ya taaluma hatua ya awali watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 1,028 kati ya hao watahiniwa 103 sawa na asilimia 10 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 925 sawa na asilimia 90.

Pia ameeleza kuwa kati ya watahiniwa 925 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 759 ambao ni asilimia 82.1 wamefaulu mitihani yao ambapo kati yao watahiniwa 348 sawa na silimia 37.6 wanastahili kutunukiwa barua za ufaulu wa mitihani na watahiniwa 411 sawa na asilimia 44.4 wamefaulu baadhi ya masomo hivyo watahiniwa 166 sawa na asilimia 17.9 hawakufaulu mitihani yao.

Aidha amesema katika hatua ya kati waliojisaliwa walikuwa 3,870 kati ya hao watahiniwa 341 sawa na asilimia 8.8 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 3,529 sawa na asilimia 91.2, kati ya watahiniwa hao 3,529 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 2,381 sawa na asilimia 67.5 wamefaulu mitihani yao kati ya hao watahiniwa 555 sawa na asilimia 15.7 wanastahili kutunukiwa barua za ufaulu na watahiniwa 1,826 sawa na asilimia 51.7 wamefaulu baadhi ya masomona watahiniwa 1,148 sawa na asilimia 32.5 hawakufaulu mitihani yao

Katika hatua ya mwisho, waliosajiliwa walikuwa 2,390 kati ya hao watahiniwa 173 sawa na asilimia 7.2 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 2,217 sawa na asilimia 92.8. Kati ya watahiniwa 2,217 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 1,169 sawa na asilimia 52.7 wamefaulu mitihani mitihani yao ambapo kati ya watahiniwa 400 sawa na silimia 18.1 wanastahili kutunukiwa barua za ufaulu na watahiniwa 769 sawa na asilimia 34.7 wamefaulu baadhi ya masomo na watahiiwa 1,048 sawa na asilimia 47.3 hawakufaulu mitihani yao.

CPA. Pius Maneno amesema Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA inatoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.

Mitihani ya muhula wa kati pamoja na ile ya Astashahada ya Viwango vya Kiamataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Taasisi za Umma (Diploma in IPSAS) itafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 19 – Ijumaa tarehe 23 Agosti 2024 na miihani ya Novemba itafanyika Jumanne tarehe 05 hadi Ijumaa tarehe 08 Novemba 2024.

Pia amewasisitiza watahiniwa kuwa mitaala mipya ya Bodi itaanza kutahiniwa kuanzia muhula wa mitihani ya Novemba 2024 na matokeo ya mitihani ya 99 ya Bodi yanapatikana kwenye tovuti ya NBAA ambayo ni www.nbaa.go.tz.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius A. Maneno

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...