NA WILLIUM PAUL, SAME.

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewaonya baadhi ya wazazi wanaotumia kesi za ukatili wa kijinsia kwa watoto kama mtaji kulipana fedha pindi anapofanyiwa ukatili.

Amewataka kuacha mara moja tabia hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea kuathiri saikolojia na afya ya mtoto pamoja na kumfanya ashindwe kutimiza ndoto zake.

Alieleza hayo kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na malalamiko ya wananchi uliofanyika Kata ya Mamba Myamba, ambapo amewasisitiza wananchi hao kutowaficha watuhumiwa wa vitendo hivyo kwenye jamii ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

“Niwaombe sana wazazi muwalinde watoto wenu, jengeni urafiki na watoto wenu ili waweze kuwaambia madhara ambayo wanayapata huko njiani wanapoenda shule na kurudi watawaambia, na bahati mbaya sisi wazazi hatuwafuatilii watoto tupo bize na kilimo cha tangawizi hatuna muda wa kukaa na watoto wetu watoto wetu wameingia kwenye hivyo vitendo wakati mwingine sio kwamba wanapenda wanatishwa na hao mabazazi”. Alisema Kasilda.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Polisi Kitengo cha dawati la jinsia Wilaya ya Same Tarafa ya Mamba Myamba inashika nafasi ya pili kati ya Tarafa sita za Wilaya hiyo kuripotiwa kwa kesi za ukatili wa kijinsia ikiwemo mapenzi ya jinsia moja (Ushoga), baadhi wa wanajamii kuficha watuhumiwa wa vitendo hivyo miongoni mwa changamoto inayochagiza kuendelea kuwepo kwa matukio hayo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...