Na Muhidin Amri,Mbinga.

SHIRIKA la Uhifadhi mazingira duniani World Wide Fund (WWF) limetoa mafunzo ya uhifadhi na elimu ya upandaji miti kwa Wanafunzi wa mikoa ya Ruvuma na Mtwara, lengo likiwa kuwapa ili kuwajengea uwezo wa kuhifadhi mazingira.

Akizungumza na Wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari kutoka wilaya za mkoa wa Ruvuma walipotembelea vitalu vya miche ya miti wilaya ya Mbinga Afisa uhifadhi wa WWF Tanzania Deogratus kilasara amesema, mafunzo hayo yanalenga kuwapa elimu na kujifunza masuala mbalimbali ya uhifadhi na upandaji miti kwa kwa kuzingatia kwamba watakuwa mabalozi wazuri katika jamii.

Amesema, lengo la shirika ni kuwapa elimu inayohusu upandaji miti kuanzia hatua ya kuandaa vitalu na miche kwani itawasaidia kuanda miti ya uhifadhi pamoja na miti ya itakayowapa manufaa mbalimbali katika jamii na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“Tunawaandaa wanafunzi hawa kuja kuelimisha na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuzuia uharibifu wa mazingira, hivyo baada ya elimu hii tunaamini uelewa wa utunzaji mazingira imerithishwa kikamilifu na italeta chachu kwa taifa” alisema kilasara.

Naye kiongozi wa msafara huo ambaye ni Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Namtumbo Osmani Mponda amesema, mafunzo hayo kwa wanafunzi ni muhimu sana kwani wao ndio wenye dhamana kwa kizazi kinachokuja hivyo kupitia mafunzo hayo kwa vitendo yataongeza wahifadhi wengi katika jamii.

“Nimefurahi kwa kuja kujifunza namna ambavyo tunaweza otesha miti kuanzia hatua ya mbegu hadi kufikia kuwa mche, tumejifunza mengi suala la uhifadhi wa mazingira naomba WWF waendelee kutoa mafunzo haya mwaka hadi mwaka kwani itasaidia kuwa na mabalozi wengi wa mazingira” alisema Mponda.

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwamba Ibrahimu Ali amesema, kupitia mafunzo hayo atakuwa balozi mzuri wa kutoa elimu, kuelemisha na kufundisha wanafunzi wenzake namna ya kuendelea kurithisha kwa vitendo katika jamii.

“Uchafuzi wa mazingira unaweza kupelekea au kusababisha mabadliko ya tabia ya nche ikiwemo ongezeko la joto duniani, hivyo ushauri wangu kwa WWF waendelee kuturithisha elimu hii kwa vitendo kwani sisi ndio taifa la baadaye”.

Naye Bahati Said mwanafunzi wa kidato cha kwanza kutoka Shule ya Sekondari ya Matemanga wilayani Tunduru, amelishukuru shirika la WWF kwa kuwapa elimu ya usimamizi na utunzaji mazingira kwani kupitia wao wataendele kuyafanya mazingira kuwa salama.

“Nimejifunza masuala ya uhifadhi mazingira kwa kuona hatua zote hiyo nimekuwa balozi bora ambaye naelewa jinsi ya uhifadhi mazingira upo hatarini kutokana na shughuli za kibinadamu kama ukataji miti ovyo, hivyo elimu hii itatuwesha kuelimisha jamii na kuyafanya mazingira kubaki salama”.
Afisa uhifadhi wa WWF Tanzania Deogratus kilasara,akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari walipotembelea vitalu vya miti wilayani Mbinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...