*Mkakati kwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme Benaco -Kyaka wa Kilovoti 220 kuanza Desemba

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuwa mkakati waliouweka katika Mkoa wa Kagera ni kuondokana na ununuzi wa Umeme nchini Uganda.

Ununuzi wa Umeme kutoka nchini Uganda ni Megawati 21 kwa mwezi ambapo Shirika linalipa sh.Bilioni 2.6 kwa kila mwezi.

Akizungumza na waandishi habari wakati kutia saini ya Mkataba na Mhandisi Mshauri (Shaker Consultancy Group ya nchini Misri) ikishirikiana na Kampuni ya usimamizi Miradi ya Umeme ya Saudi Arabia(DC) Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amesema katika kuimarisha hali ya upatikanaji umeme katika Mkoa huo kuweka mikakati ya kuwa na vyanzo vya ndani vya kuzalisha Umeme.

Amesema Shirika limesaini mkataba kwa ajili ya kuandaa nyaraka za manunuzi ya wakandarasi wa ujenzi pamoja na usimamiziwa ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme ya msongo wa Kilovoti(220) ya Benaco hadi Kyaka Mkoani Kagera.

Amesema kuwa ujenzi wa njia hiyo ya kusafirisha umeme ya Benaco katika Mkoa wa Kagera kwa kuwezesha Wilaya za Kyerwa,Karagwe,Misenyi,Muleba,Bukoba vijijini na Manispaa ya Bukoba na kuunganishwa katika Gridi ya taifa ya Kituo cha Benaco Wilaya ya Ngara pamoja na kituo chakupoza umeme cha Kyaka Wilaya ya Misenyi.

Aidha amesema kuwa Mkoa wa Kagera kwa kipindi kirefu katika Wilaya za Kyerwa,Karagwe,Misenyi, Muleba,Bukoba vijijini na Manispaa ya Bukoba zimekuwa zikipokea kilovoti 132 kutoka nchini Uganda kupitia kampuni ya kusafirisha umeme ya(UETCL).

Amesema ujenzi wa mradi huu utagharimu kiasi cha Dola za kimarekani Milioni 135.4 ukihusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme ya umbali wa kilometa166.17 kutoka Benaco mpaka Kyaka, kipya kituo cha kupoza umeme Kyaka kilichopo sasa.

Hata hivyo amesema fedha hizo za ujenzi zitagharamiwa na Serikali Bilioni 6.2 ,Mfuko wa Maendeleo wa Saudi (SFD) Dola za Marekani Milioni 13,Mfuko wa Maendeleowa Abudhabi Dola za Marekani Milioni 30 na Mfuko wa Maendeleo ya Kimataifa wa OPEC ambao utachangia kiasi cha Dola milioni 60 za Marekani.


Mhandisi Nyamo-Hanga amesema maandalizi ya mradi wa Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa Benaco-Kyaka(220kVna vituo vya kupoza umeme) utasimamiwana Mhandisi Mshauri Shaker Consultancy Group ya nchini Misri pamoja na TANESCO.

Amesema mkandarasi wa ujenzi huo unatarajiwa kuanza mwezi Disemba 2024 na utekelezaji wa mradi utakamilika ndani ya miezi 24 (2026) Mhandisi Mshauri Shaker Consultancy Group ya nchini Misri Dkt.Ismail Shaker amesema kuwa ujenzi huo utanaza kutokana na mkataba huo na utamalizika kwa wakati.

Amesema kuwa mradi huo mkandarasi atapatikana na kazi hiyo itakwenda kama ilivyopangwa katika kutekeleza matakwa mkataba
 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi  Gissima  Nyamo-Hanga akizungumza mara baada ya kusaini Mkataba na Mkandarasi Mshauri wa Shaker Consultancy Group wa Ujenzi wa Kituo cha Kusafirishia Umeme Benaco hadi Kyaka mkoani Kagera hafla ya kutiliana mkataba huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
 

Mkandarasi Mshauri wa Shaker Consultancy Group Dkt.Ismail Shaker kuhusiana na ujenzi  wa Ujenzi wa Kituo cha Kusafirishia njia ya  Umeme Benaco hadi Kyaka mkoani Kagera hafla ya kutiliana mkataba huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
 

Picha ya pamoja kati TANESCO na Shaker Consultancy mara baada ya kusaini Mkataba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...