Na Mwandishi Wetu

Baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Mohammed Ali Kawaida kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kufungia Mtandao wa X ambao Zamani ulijulikana kama Twitter kutokana na mtandao huo kuruhusu mambo ambayo ni kinyume na Utamaduni wa Watanzania

Jukwaa la wanahabari wa mitandao ya Kijamii Tanzania(JUMIKITA) limeiomba Serikali ya chini ya Uongozi makini wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokubali kamwe kuingia kwenye mtego wa kufungia mtandao huo wa Kijamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mweyekiti wa Jukwaa hilo amesema kuwa wakati wa sasa kufungia Mtandao sio jambo linalojenga afya kutokana na kuongezeka mifumo ya Teknolojia ya upatikanaji wa taarifa.

"Ni kama ilivyo Instagram ,Facebook na YouTube, 'x' au Twitter ni sehemu ambayo vijana wa Kitanzania wamekua wakilitumia Jukwaa hilo kujipatia riziki mfano Matangazo lakini pia hata Kazi nzuri za Serikali mbalimbali Wanahabari wa mtandaoni wamekua wakizichapisha 'x' "

"JUMIKITA ipo tayari kushirikiana na Serikali kujua namna bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii na inatoa ushauri serikali isiingie kwenye mtego wa kufungia mtandao huo"amesema Matwebe
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA)Shaban Matwebe pichani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...