Msanii anayekuja kwa kasi, kutoka Nigeria, Vasa amerejea kwa kishindo, kwa kuachia wimbo wake mpya uitwao "Trabaye", ambao amemshirikisha msanii wa muziki kutoka lebo ya Mavin, Crayon.

Wimbo huu ni miongoni mwa ngoma za mkali huyo zilizopo kwenye project yake ijayo iitwayo Vasa, Book Of Vasa’’ ambayo itatoka wiki chache zijazo.

Vasa anayejulikana kwa nyimbo zake za silky na kuwa na uwezo kwa kupita kwenye kila mdundo. Akiwa amesainiwa na Ize Records,mkali huyu asisimua vyema wapenzi wa muziki kwenye ngoma kama "Bolanle" na "Treasure". Wimbo wa Vasa uitwao "50-50," ni miongoni mwa nyimbo bora zaidi kutokea na kufikisha streams 200,000 kwenye Spotify, na kusababisha remix ya kuvutia. ambayo alimshirikisha Bella Shmurda.

Kufuatia mafanikio yaliyoenea ya remix yake "50-50" na Bella Shmurda, Vasa inaendelea kusukuma mipaka na kuonyesha ustadi wake. Akiwa na umri wa miaka 19 tu, Vasa, mzaliwa wa Freedom Ali, tayari amejitengenezea nafasi katika anga ya muziki ya Nigeria. Uwezo wake wa kipekee wa kuchanganya Afrosoul na sauti za kisasa umemfanya awe na mashabiki lukuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...