Na Mwandishi Wetu

VIONGOZI mbalimbali wa Serikali wametembelea Banda la MSD kwenye maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 June, 2024.

Miongoni mwa viongozi waliotembelea ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo George Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Ridhiwani Kikwete (Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Akizungumza akiwa katika banda hilo Waziri Simbachawene amesema anafurahishwa na namna MSD inavyotekeleza majukumu yake katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya “nimefurahishwa na namna MSD ilivyosambaza mashuka kwenye majimbo yetu ambayo yamesaidia katika utoaji wa huduma za afya”

Ameipongeza pia MSD kwa kupeleka haraka Jokofu la kuhifadhia miili Kituo cha Afya Kibakwe – Mpwapwa - Dodoma ambalo lilikuwa linahitajika kwa kiasi kikubwa.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...