Na Mwandishi Wetu

Wadau wa afya katika Mikoa ya Kagera na Geita Waaswa kulipa madeni wanayodaiwa na MSD, yanayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 6.5, ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa weledi katika kununua, kutunza, na kusambaza bidhaa za afya.

Sambamba na kulipa washitiri wanaofanya nao biashara, ili kuufanya mnyororo wa upatikanaji wa bidhaa za afya nchini usikatike, bali uwe endelevu.

Rai hiyo imetolewa hapo na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa MSD na Wateja wake, kutoka Mikoa ya Kagera na Geita, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, uliofanyika katika Ukumbi wa ELCT ulioko Manispaa ya Bukoba Mkoani humo.

Erasto amesema uwepo wa limbikizo kubwa la madeni linalodaiwa na MSD kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, unaathiri kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa taasisi hiyo, hivyo kukwamisha uwezo wake kutoa huduma, kutokana na kuzidiwa na mahitaji kunako sababishwa na uhaba wa fedha.

Katika hatua nyingine amewataka wadau hao kuendelea kushirikiana kwa kuboresha mahusiano na mawasiliano baina yao, ili kwa pamoja waweze kujadiliana na kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili na kuathiri mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwenye maeneno yao.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa MSD Victor Sungusia, amesema MSD imefanya maboresho huduma zake kwa kiasi kikubwa ikiwemo upatikanaji wa bidhaa za afya ambapo hivi sasa uwezo MSD kukidhi mahitaji ya wateja wake upanda kutoka asilimia 40 kwa mwaka 2021/2022, hadi kufikia asilimia 80 kwa mwaka 2023/2024, jambo ambalo limepunguza uhaba wa bidhaa na malalamiko ya wateja.

Sungusia ameeleza pia jinsi MSD ilivyoboresha jukumu lake la uhifadhi kwa ujenzi wa maghala mapya kwenye kanda zake nchini, ambapo hivi sasa ujenzi wa maghala kwenye kwenye kanda za Dodoma, Mtwara unaendelea kwa bajeti ya fedha ya m waka 2023/2024 na kuanzia mwaka ujao
wa fedha maghala kwenye kanda za Kagera na Mwanza unatazamiwa kuanza.

Katika hatua nyingine Sungusia amebainisha jinsi MSD ilivyoboresha usambazaji wa bidhaa za afya nchini, kutoka mara 4 hadi kufikia mara 6 kwa mwaka, ambapo zoezi hilo hufanyika kila baada ya miezi miwili, huku maboresho hayo yakielezwa kuimarisha hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

Naye Meneja wa MSD Kanda ya Kagera Masatu Kalendero amewashukuru wadau hao kwa ushirikiano wao, huku akiahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizoibuliwa huku akiwashi wadau hao kuendelea kudumisha umoja na ushirikiano, ili kwa Pamoja waweze kuboresha afya kwa wananchi.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...