Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) Editruda Lukanga akizungumza wakati ufunguzi wa warsha ya siku moja kwa wanahabari na wadau mbali mbali wa masuala ya Hali ya hewa ikiwemo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam Juni 4, 2024.
Ofisa uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Monica Mutoni akifafanua jambo wakati wa warsha ya siku moja kwa wanahabari na wadau wa Hali ya hewa. Warsha hiyo iliyoandaliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) imefanyika jijini Dar es Salaam Juni 4, 2024.



Meneja Mradi wa kuzuia kuzama maji Ziwa Victoria, Arthur Mgema akionyesha kifaaa cha uokozi kinachomsaidia mtu kutozama kwenye maji wakati wa warsha ya siku moja ya wanahabari na wadau wa hali ya hewa wakiwemo TMA. Warsha hiyo iliyoandaliwa na EMEDO imefanyika Juni 4,2024 jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la usimamizi wa Mazingira na Maendeleo ya Uchumi (EMEDO) limesema kuwa takwimu za shirika la afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa zaidi ya watu laki mbili kwa mwaka wanakufa kutokakana na kuzama maji.

Hayo yamesemwa Juni 4,2024 na Mkurugenzi wa Shirika hilo Editruda Lukanga wakati wa warsha ya siku moja ya wanahabari na wadau mbalimbali wa masuala ya Hali ya hewa ikiwemo Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na kusema kuwa kuna haja ya kushirikiana kwa pamoja ili kutoa elimu ambayo itasaidia kuzuia watu hasa wavuvi kufa maji.

Amesema katika ripoti hiyo ya WHO inaonyesha asilimia 90 ya vifo hivyo vinatokea katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo ni wakati muafaka sasa kwa nchi kuchukua hatua hususani katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa yakitokea.

Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanakufa maji kutokana na uzembe hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari ya maji yatokanayo na mvua kubwa, mito, maziwa na bahari kwani kwa kuwa yanaua na kuacha simanzi kwa familia, jamii na Taifa Kwa ujumla.

"Ni wakati sasa wa kuleta mabadiriko na kuchangia usalama wa namna tunavyotumia maji". Amesema

Kwa upande wake, Ofisa uhusiano wa TMA, Monica Mutoni amesema wanashirikiana vema na shirika hilo la EMEDO na wadau wengine ili kuzuia watu kupata na changamoto mbaya za mabadiliko ya Hali ya hewa ukizingatia kuwa watu wanaofanya shughuli zao katika maziwa makuu na ukanda wa bahari wanakumbana na athari za Hali mbaya ya hewa hususani upepo mkali.

"Kama mnavyofahamu TMA sisi jukumu letu kutoa taarifa za hali ya hewa na moja ya jukumu letu ni kutoa taarifa za hali ya hewa upande wa sekta ya uvavi tunashirikiana na wenzetu Imedo kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinawafikia wavavi" alisema.

"Wenzetu wanaofanya shughuli zao kwenye ukanda wa bahari na maziwa makuu wanapata changamoto nyingi kutokana athari za hali ya hewa hususani upepo mkali na sisi TMA tumetoa tabiri za msimu wa Juni mpaka Agosti kuwa kitakuwa kipindi cha kipupwe kutakuwa na upepo mkali kwa baadhi ya siku ambazo tutakuwa tukitoa taarifa hivyo upepo huo utaleta athari upande wa bahari na maziwa kwa hiyo tutashirikiana na wenzetu kuhakikisha zinawafikia wahusika kwa wakati na kuchukua hatua stahiki"

Amesema kuwa TMA itaendelea kutoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa vipindi vya kila siku kwa lengo la kuokoa mali na maisha ya wananchi.

Naye Meneja Mradi wa kuzuia kuzama maji Ziwa Viktoria Arthur Mugema amewashauri watu wanatumia bahari, mito na maziwa wakiwemo wavuvi kuhakikisha wanakuwa na vifaa maalumu vya kuogelea kama vile mambo ya okozi ( life Jacket) na kuwafanya wasizame maji pindi vyombo wanavyotumia vinapopata hitilafu na kuiomba Serikali kuona umuhimu wa kupunguza gharama za vifaa hivyo.

Amesema, mwaka 2021 walifanya utafiti wa kwanini kuna ajari nyingi za wavuvi kuzama ziwani na mtazamo wa wavuvi, jamii na viongozi kule chini pamoja na madhala wanayopata familia ambayo imempoteza mtu wanayemtegemee.

Amesema kuwa katika utafiti wao waligundua kuwa wavuvi wana uelewa hafifu juu ya matumizi ya vifaa vya uokoaji na hawapati taarifa za hali ya hewa kwa wakati.

"Tulibaini kuwa wavuvi wanauelewa mdogo kwenye elemu ya usalama kwe ye Mji , matumizi ya vifaa maboya okozi wavuvi wachache wanaovaa ijapokuwa sheria inawataka wavae,.... changamoto nyingine ni upatikanaji wa maboya okozi pamoja na gharama zake zimekuwa kubwa. " alisema.

Amesema, baada ya kubaini changamoto hizo ndipo wakaja ma mradi mradi wenye lengo la kupunguza ajali za wavuvi kuzama katika Ziwa Victoria mradi ambao unatekelezwa kanda ya Ziwa katika Mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara.

"Mradi huu ulioanza mwakan 2022 mpaka 2025 tukilenga kuwabadilisha wavuvi mtazamo na kutoa elimu juu ya matumizi ya maboya okozi ambapo mpaka sasa tumekwisha anza kutengeneza maboya okozi yatakayowawezesha wavuvu kukaa muda mrefu kwenye maji"

Ameiomba serikali kupunguza kodi ya uingizaji vifaa hivyo ili vipatikane kirahisi ili kupunguza ajali hizo.

Amesema kuwa lengo kubwa la mradi huo ni kusapoti maendeleo ya uchumi wa Bluu kwa kuwa usalama wa nguvu kazi ya utendaji huo.

Aidha ameeleza kuwa mbali na kutoa elimu kwa wavuvi wanatoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari zilizoko katika Maeneo yaliyoko Kanda ya Ziwa Kwa kuwa walengwa wakubwa ni wavuvi, watoto na akina mama wachakatani wa samaki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...