Waziri Kassim Majaliwa Leo Juni 21, 2024 amekutana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Katibu wa Kamati ya CPC Jimbo la Shanxi nchini China.

Katika mazungumzo yao ambayo yamefanyika kwenye Ofisi ndogo za Waziri Mkuu, Magogoni Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa amesema kuwa Tanzania itaendeleza mahusiano na China kwenye maeneo ya Siasa, Kijami na Kiuchumi.

Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi kiliwakilishwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (MCC) Ndugu. Rabia Abdalla Hamid.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...