Mwandishi wetu.Babati
Taasisi
ya Uhifadhi na Utalii ya Chem Chem Safaris, iliyopo eneo la hifadhi ya
jamii ya wanyamapori ya Burunge(Buruge WMA), wilaya Babati Mkoa wa
Manyara,imeshinda tuzo ya utalii na Uhifadhi unaoshirikisha jamii.
Tuzo
hiyo, imetolewa na Taasisi ya kimataifa African Travel and Tourism
Association(ATTA) ya nchini Uingereza, ambayo ilishirikisha nchi mbali
mbali duniani.
Akitangaza
ushindi wa chemchen Rais wa ATTA, Nigel Vere Nicoll, alisema walipokea
idadi kubwa ya taasisi binafsi za Utalii na Uhifadhi, ambazo
zinafanyakazi na jamii ili kupokea tuzo katika vipengere vinane ambavyo
vinatambulika na shirikisho la Utalii duniani.
"Baada
ya majaji kupitia sifa za kila taasisi na pia kupokea maoni kutoka kwa
watalii waliotembelea maeneo hayo, Taasisi ya Chemchem ndio ilikuwa
mshindi wa kwanza wa jumla kutokana na kuweza kushirikisha jamii katika
eneo la Burunge WMA katika uhifadhi na Utalii na jamii kunufaika
"alisema
Taasisi nyingine
zilizotangazwa kushinda, katika utoaji wa tuzo hizo uliofanyika London
uingereza ni kutoka nchi za Uingereza, Namibia, Kenya na Botswana.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Meneja Mkuu wa Taasisi ya Chem Chem, Clever
Zullu alisema ushindi wa tuzo ya Uhifadhi na Utalii unaoshirikisha
jamii, ambao wamepata umetokana na jitihada kubwa za Serikali na wadau
wengine kukuza sekta ya utalii na uhifadhi nchini.
"Tunashukuru
Chemchem kwa kupata tuzo hii ambayo ina maana kubwa sana katika
shughuli zetu za Utalii na uhifadhi, ambao unashirikisha jamii kwa kiasi
kikubwa"alisema
Zullu
alisema ushindi huo ni matokeo pia ya kazi nzuri ya Rais Samia Suluhu
kufungua nchi katika Utalii na kuvutia maelfu ya watalii duniani kuja
Tanzania.
"Chem chem
tutaendelea kushirikiana na serikali na taasisi za utalii na uhifadhi za
TANAPA, TAWA, TAWIRI lakini pia Burunge WMA kuendeleza utalii na
uhifadhi katika eneo hili kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo"alisema.
Kwa
upande wake, Meneja wa hotel ya chemchem, Elizabeth Omboi na mkuu wa
Idara ya huduma mbali mbali katika hotel hiyo,Peter Corneli walisema
ushindi huo, una maana kubwa kwao na utavutia watalii zaidi.
"Tumekuwa
tukifanya shughuli za utalii wa hapa kwa kushirikisha jamii, tunatoa
misaada kusaidia sekta za elimu, afya, mazingira na hata kusaidia
makundi ya akina mama katika ujasiriamali"alisema Omboi.
Kwa
upande wake, Corneli alisema miongoni mwa sababu nyingine ambazo
zimekuwa zikivutia watalii kutembelea katika hoteli zao ni kupata
chakula cha asili ya Kitanzania ambacho kimeandaliwa vizuri na kupata
fursa ya kutembea kwa miguu katika maeneo ya wanyamapori ikiwepo kufika
eneo la ziwa Manyara na kuona machweo na mawio ya jua.
Katibu
Mkuu wa Burunge WMA, Benson Mwaise, alisema ushindi wa Chemchem ni
ushindi wa Burunge WMA kwani, chem chem ni miongoni mwa taasisi ambazo
zimewekeza katika eneo hilo.
"tumepata
faraja kutokana na ushindi huu, dunia imetambua jitihada zetu katika
uhifadhi lakini pia jamii inavyoshirikisha katika shughuli za Utalii na
uhifadhi hili ni jambo kubwa sana"alisema
Taasisi
nyingine ambazo zimepata tuzo hizo za hapa nchini ni Kisiwa cha chumbe
kilichopo Zanzibar,Taasisi ya Asilia Afrika ya Uingereza, Lemala Camps
and Lodges Tanzania.
Taasisi
nyingine ni African Monarch Lodges ya Namibia,How Manyt Elephant ya
Uingereza, Gamewatchers Safari&Porini Camp ya Kenya na Lets Go
Travel Uniglobe ya Kenya.
Tuzo
hiyo ya chemchem kama mshindi wa kwanza inatarajiwa kuwasilishwa nchini
hivi karibuni na kushuhudiwa na serikali na wadau wa sekta ya utalii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...