Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia miongozo yake imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba watafiti wa kike wanapewa kipaumbele pale panapowezekana na watafiti wachanga wanapewa upendeleo maalumu kwani utafiti huo wanaufadhili katika malengo ya umahiri.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya sayansi na Teckonolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu wakati wa ziara iliyofanywa na kamati ya kitaifa ya ushauri kuhusu utekelezaji wa programu ya kizazi chenye usawa katika Tume hiyo iliyoanza Julai 9 mwaka huu na kutegemewa kumalizika hapo kesho ambapo imetekelezwa katika mkoa wa Dodoma , Dar es Salaam pamoja na Unguja .

“Leo tulikuwa na kamati ya julwaa la usawa wa kijinsia hapa kwetu COSTECH na tumeongea nao mengi kuhusiana na jukwaa la usawa wa kijisnia kubwa kuwaambia kuwa COSTECH tunafanya nini hasahasa katika masuala haya ya usawa”

“Kuna nia mahususi ya kusema kwamba hawa watafiti changanga pia wapewe fursa na wao siku moja wawe mahiri”

Kwenye suala la ubunifu Dkt. Nungu amesema wanatoa taarifa kwamba pamoja na msuala kwamba wantoa huduma kwa wabunifu wote kwa ujumla lakini kupitia ukumbi wetu wa kiubunifu wabuni wanapogramu maalumu ambayo inaitwa bunidivas inayoangalia mabinti katika kuwasaidia kwenye masuala ya ujasiliamali ambapo kila mwaka wanawachukua wanafunzi na kuwapa fedha kwaajili ya kuendeleza bunifu zao.

vilevile Nungu amesisitiza kwamba Wanafunzi washirikishwe kwenye kujitambua na kutambua kwamba kunafursa kwenye ubunifu.

Kwa upande wake , Mjumbe wa Kamati ya ushauri ya kizazi chenye usawa , Grace Munisi amesema COSTECH wamejitahidi kwenye programu zao hasa zile za kuweza kumkwamua mwanamke kiuchumi ambazo zimepewa nafasi maalumu za kuiangalia kuanzia jinsi wanavyofanya udahili , tafiti na miradi mbalimbali ya kuweza kuzingatia masuala mazima ya jinsia na kuangalia mwanamke na kijana anaangaliwa.

Aidha kupitia ziara hiyo, kamati pia ilipata nafasi ya kutembela kituo cha makuzi na malezi ambapo Munisi alisema walimu wengi wameamua kujitolea kufundisha watoto katika kituo hicho na kuonesha jinsi serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaweza kufanya agenda hiyo ikafikia malengo makubwa zaidi.

“Tunamshukuru Rais samia kwa kuliona hili na kutuagiza sisi kuja kuhakikisha kwamba hivi vitu vinafanyika katika viwango vinavyotakiwa na wananchi wenyewe wnaaelewa programu, pia wanaruksa ya kushiriki na kuonyesha matokeo ambayo wananchi wenyewe wameyafanya kwa serikali yao”

Naye Mwalimu wa watoto wadogo katika kituo cha muongozo cha maelzi na makuzi ya awali kwa mtoto kuanzia miaka 3-5, Martha Njogoro ameiomba kamati hiyo na serikali kwa ujumla kusaidia katika ujasiriamali wa wakina mama wanaoleta watoto wao katika kituo hicho kwani wengi wanauchumi mdogo

vileviloe ameiomba serikali kuboresha vifaa kwa kupeleka vifaa vya kutosha vya kuchezea watoto katika kituo hicho kwani wamejikita zaidi katika ubunifu wa michezo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...