Wakati Maonyesho ya 48 ya biashara ya kimataifa yakifunguliwa na mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi aliyeambatana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, walitembelea mabanda mbali mbali kabla ya kufungua rasmi.

Miongoni mwa makampuni yaliotembelewa na Maraisi hao ni banda la kampuni ya GF Group ambao ni wauzaji wa magari na mitambo.

Akizungumza wakati Marais hao wakitembelea banda lao, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd , Imrani Karmali alisema wao baada ya ziara ya Rais nchini Korea kushawishi wawekezaji kuwekeza nchini,wao kupitia kiwanda chao cha kuunganisha magari cha GF Assembling wamezungumza na wakorea na wako tayari kuja kuunganisha magari hayo aina ya Hyundai nchini.

Akaeleza zaidi kuwa lakini wamewataka kampuni ya GF kuwa na oda zaidi ya magari 300 kwa kuanzia, ndipo Wakorea hao watoe idhini ya kufunga kiwanda cha kuunganisha magari hayo.

"Na sisi kama GFA tupo tayari lakini tunaiomba Serikali kupitia Wizara na tasisi zake kutuunga mkono katika hili kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa na la uhakika la kuanzia na matunda ya ziara yako nchini korea kuonekana kwa Hyundani kutengenezwa nchini Tanzania"Alimaliza Karmali.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...