Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke (TRRH) imepokea rasmi magari mawili ya kubeba wagonjwa, ambayo yamezinduliwa na Mhe. Dorothy Kilave, Mbunge wa Jimbo la Temeke. Ujio wa magari haya yanaenda kuboresha huduma za rufaa na za dharura zilizopo hospitalini hapo, na kufanya idadi ya magari ya kubeba wagonjwa kuwa matano.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Joseph Kimaro, amethibitisha maboresho haya wakati akiwasilisha taarifa fupi ya utendaji kazi na maboresho katika hafla ya ugawaji wa magari ya kubeba wagonjwa mbele ya mgeni rasmi, Mhe. Dorothy Kilave. Dkt. Kimaro ameeleza mafanikio mbalimbali ya hospitali hiyo moja ikiwa ni kununua kifaa tiba kinachoitwa laparoscopy tower, ambacho kitawezesha hospitali kufanya upasuaji kwa njia ya tundu ndogo, hivyo kupunguza rufaa ya wagonjwa kwenda katika hospitali za juu.

 Aidha, kupitia utendaji mzuri wa timu ya uendeshaji wa huduma za afya, hospitali imeanza kutoa huduma za usafishaji damu (dialysis), na ndani ya wiki kadhaa imefanya sesheni 28 kwa wagonjwa nane waliopatiwa huduma. Kwa upande wake, Mhe. Dorothy Kilave amepongeza juhudi za hospitali katika kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi. Amesema kuwa kila anapofika hospitalini hapo anakuta kuna maboresho mapya ambayo wananchi wa Temeke wamekuwa wakiyatamani. 

Mhe. Kilave ametoa shukrani na pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Mhe. Rais kwa kusaidia na kusikiliza mahitaji ya majimbo mengi. Ameongeza kuwa, kwa siku ya leo, tunashuhudia Jimbo la Temeke likipokea vifaa hivi vya magari ya kubeba wagonjwa. Aidha, maboresho na mafanikio haya yanatupa moyo kuona kuwa kweli kazi zinafanyika. Pia, amehakikishia uongozi juu ya uwepo wa fedha zitakazowezesha ujenzi wa gorofa sita litakalosaidia kupunguza na kuondoa changamoto ya ufinyu wa eneo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...