Na Mwandishi Wetu

JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma amesema uwepo wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) na utekelezaji wa sheria ya ushindani vinalenga kuzuia athari za ukiritimba katika soko pamoja na kuondoa vizuizi vya uwekezaji katika maeneo mbalimbali.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipotembelea banda la FCC katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba mesisitiza kuwa sheria ya ushindani ni msingi wa ustawi na uchumi katika nchi zilizoendelea.

Prof. Ibrahim amesema kuwa licha ya FCC kuzuia athari za ukiritimba katika soko pia hurekebisha na kuwachukulia hatua wale wote wanaokikuka Sheria ya Ushindani, pamoja na kufanya biashara ya bidhaa bandia.

"Nawapongeza sana FCC kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kusimamia ushindani wa kibiashara unaopelekea kuvutia uwekezaji nchini."amesema Prof. Ibrahim.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma (FCC) Bi. Roberta Feruzi alipotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es Salaam.Maofisa wa FCC wakitoa elimu kwa wanachi waliotembelea banda la FCC wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...