Mgombea Urais TLS, Sweetheart Nkuba akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua kampeni zake ambapo pia ametangaza dira zake kabla ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Mapema mwezi Agosti, mwaka huu wa 2024 jijini Dodoma


WAKATI Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kikijiandaa na uchaguzi ujao wa urais unaotarajiwa kufanyika tarehe 2, Agosti mwaka huu, wagombea mbalimbali wanaowania nafasi hiyo wameeleza vipaumbele vyao na maono yao juu ya nafasi hiyo.

Wakili Sweetbert Nkuba akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 10,2024 ameeleza dhamira yake ya kuwaunganisha mawakili wote nchini na kulinda haki na maslahi yao iwapo atachaguliwa.

Amesema TLS iliundwa kwa lengo la kuwaleta pamoja mawakili, kutetea na kusimamia haki zao bila kuangalia ukomavu au uchanga wa mtu yeyote.

“Lengo langu ni kuimarisha TLS kwa kukuza umoja kati ya mawakili wote, kuhakikisha haki zao zinazingatiwa bila kuzingatia umri wala uzoefu,” ameeleza.

Nkuba amesisitiza mpango wake wa kuunga mkono mawakili vijana ambao mara nyingi wanakabiliwa na kutengwa .

"Ikiwa nitachaguliwa, ninakusudia kuanzisha kituo cha ukuzaji kwa wanasheria wachanga ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto za utendaji wa kisheria," amesema.

Aidha Nkuba amependekeza kushirikiana na taasisi za fedha kuanzisha mpango wa kuruhusu mawakili kulipa ada za mwaka za TLS kwa awamu.

Nkuba amesema, atasimamia maslahi ya mawakili kwani ili wakili aweze kulipa ada ni lazima kibali chake kifanye kazi anaposhindwa kulipia basi hapati maslahi tena hivyo ataishauri serikali iangalie upya namna ya kusaidia wakili ambaye hajaweza kulipa ada ikiwemo kulipa kidogo kidogo kwa kiasi atakachokuwa nacho kwa wakati huo ili aweze kuendelea kutoa huduma alafu kiasi kingine atalipia baadae ama serikali kama itaridhia inaweza kukamilisha hili na hii itasaidia kupunguza vijana wasio na ajira mitaani,"amesema

Amesema kuwa akiwa Rais wa TLS atahakikisha kila wakili anapata bima ya afya "Tunalenga kutoa huduma kamili ya afya kupitia ushirikiano na watoa huduma za bima, kuruhusu wanachama kulipa malipo kwa awamu zinazoweza kudhibitiwa," .

Pia Nkuba amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa TLS atahakikisha heshima ya chama hicho inarejea na kuwa yenye nguvu kwani kumekuwa na mambo ambayo yanatishia kuwagawa mawakili kutokana na shughuli wanazozifanya huku pia wakiwemo wenye itikadi za vyama hivyo kutaka kuihamisha TLS kutoka kwenye uhalisia wake na kutaka kuifanya kuwa chama cha siasa jambo ambalo halikubaliki.

Amesema kuwa atawasaidia vijana chipukizi ambao wamekuwa wakibaguliwa kwa kutopewa ushirikiano na mawakili wakongwe baada ya kuwa wameapishwa tayari kuwa mawakili,hivyo ataandaa Ofisi itakayojumuisha mawakili wote ili kama kuna wakili atakuwa na kazi ya kufanya anapotoka ataambatana na chipukizi ma hivyo kuwapatia mwanga wa namna ya kufanya kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...