TUME ya Ushindani nchini (FCC) imesema itahakikisha Mwananchi nchini haumizwi na bidhaa zisizo na ubora ikiwemo kusimamia sheria ya ushindani nchini inayodhibiti bidhaa hizo.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa FCC, William  Erio,wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la FCC lilopo kwenye maonesho ya 48 ya sabasaba yanayoendelea jijini hapa.

Erio amesema FCC imejitahidi kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya kuepuka Bidhaa Bandia.

"Majukumu yetu pia ni kutoa elimu kwa watu kutofanya Biashara Bandia na kuhalibu ushindani wa biashara,sisi FCC tutaendelea kuchukua hatua"amesema Erio.

Erio,amewataka wafanyabiashara na wawekezaji kabla ya kufanya biashara nchini watembelee FCC kwa lengo la kupata elimu .

"Na sisi tunatumia maonesho haya pamoja na kueleza kazi kwa Umma,tunatumia maonesho haya pia kunawashauri kutofanya Biashara Bandia pamoja kutoweka bei kubwa itakayomuumiza mlaji,"

"Tunawakaribisha kwenye Banda hili ,na sisi tutatoa elimu kipindi chote cha maonesho"Amesema Erio.

Hata hivyo,Erio,amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji kutokana na sera nzuri ikiwemo kuwepo kwa mamlaka inayodhibiti bidhaa bandia ikiwemo FCC.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...