Na Mwandishi wetu, Mirerani
MWENGE
wa uhuru umezindua mradi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu
matatu ya vyoo vya shule ya sekondari Mirerani B.W.Mkapa iliyopo Kata ya
Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, uliogharimu shilingi
61,560,500.
Mkuu wa shule
hiyo Samwel Kaitira akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya mwenge wa
uhuru, amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 56 ni fedha za
Serikali kuu na shilingi milioni 5.6 ni nguvu za wananchi.
Kaitira
amesema mradi huo una uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 wa kidato cha tano
kwa mkupuo mmoja na kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha kwanza
hadi cha nne, kuamsha ari ya kusoma kwa bidii na kupunguza mdondoko.
Amesema
mradi huo ulianza mwezi Februari mwaka 2024 na mradi umetekelezwa kwa
fedha za serikali kwa mwaka 2023/2024 na nguvu za wananchi kupitia
mafundi wa ndani.
“Tunapenda
kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu
Hassan, kwa kutupatia fedha zilizotekeleza mradi huu na tunampongeza kwa
kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo, tunasema kazi
iendelee,” amesema Kaitira.
Kiongozi
wa mbio za mweng wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024, Godfrey Eliakim Mzava
amepongeza mradi huo kwani utaongeza idadi ya vijana nchini kupata
elimu ya kidato cha sita.
Mzava
amesema mwenge wa uhuru wa uhuru unazindua madarasa hayo kwa lengo
husika na kutoa rai kwa vijana watakaoyatumia madarasa hayo wasome kwa
bidii ili waelewe masomo na kufaulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...