Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar Es Salaam leo tarehe 5 Julai, 2024.

Aidha, amehimiza watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kutatua changamoto za wananchi wanaotembelea banda hilo kwa ajili ya kupata huduma na uelewa masuala yanayotekelezwa na ofisi hiyo.

Katika Maonesho hayo Naibu Katibu Mkuu ametembelea Idara, Vitengo na Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kujionea namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo katika maonesho hayo.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...