Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi, ametembelea banda la NSSF katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama SabaSaba na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutokana na kupata mafanikio mbalimbali katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Aidha, Mhe. Ndejembi alijionea NSSF inavyotoa elimu ya hifadhi ya jamii, usajili wa wananchi walio katika sekta isiyo rasmi, mifumo ya TEHAMA, mapambano dhidi ya rushwa, miradi ya uwekezaji na huduma za NSSF kidijitali.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...