Baadhi ya matukio katika Maonesho ya Sabasaba


Bima hiyo inatoa hadi mkopo wa Nisogeze kupitia simu ya kiganjani

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

NIC insurance yaja na Bima ya Maisha ya Maajaliwa ya kuingia mkataba na Mteja kwa kipindi cha miaka mitano hadi 30.

Bima ya Maisha ya Maajaliwa inatoa dhamana ya kifedha kwa mteja au wategemezi WA mteja  endapo mteja atamaliza mkataba wake au akipatwa na janga la kifo kabla ya kumaliza mkataba wake.

Akizungumza katika Maonesho ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Afisa Bima wa NIC Deogratius Mlumba amesema bima ya Maisha ya Maajaliwa  mteja anapata fursa tatu kwa wakati mmoja  kwanza kupata ya kujiwekea akiba kulingana na malengo yake ya kupata faida kutokana na akiba yake pili kulinda wategemezi wake endapo atapatwa na janga la kifo.

Mlumba amesema faida ya Bima hiyo inatoa mafao ya Bima ya Maisha yanayozingatia thamani ya mfumko wa bei  kwa kulipa zaidi kiasi alichochangia mteja.

Aidha amesema endapo Mteja atapatwa na kifo familia yake itapata fidia ya asilimia 100 ya thamani ya Bima 

Hata hivyo amesema Bima ya Maisha ya Maajaliwa ina mafao moja ni mafao ya ukomo pili mafao ya kifo endapo mteja atapatwa muda wowote ndani ya mkataba.

Amesema katika mafao ya kifo ni fidia inayolipwa kwa wategemezi endapo mteja atafariki muda wowote baada ya kujiunga na Bima ya Maajaliwa.

Mlumba amesema mafao ya kumaliza mkataba ni mafao ambayo yatalipwa kwa mteja endapo atamaliza muda wake wa mkataba wa Bima ya Maisha ya Maajaliwa.

Amesema mteja akishindwa kuendelea kuchangia Bima anaweza kufanya yafaatayo moja ni kupunguza thamani ya Bima ili aweze kuendelea  kuchangia au anaweza akaacha kuchangia na kusubiri mpaka ukomo wa mkataba wake.

Bima ya Maajaliwa mteja anaweza kunufaika kwa kupata mkopo nafuu wa Nisogeze kwa kutumia simu yake ya kiganjani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...