Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi waliotenguliwa ni kama ifuatavyo:-


  1. B.i Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolph Ulanga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).


  1. Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania na Bw. Maharage Aly Chande, Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania.


  1. Prof. John Nkoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Bi. Justina Tumaini Mashiba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).



Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...