BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzindua Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) ambao umelenga ifikapo 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia Shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO,) pamoja na Taasisi ya Kuendeleza Huduma za Nishati Endelevu (TaTEDO,) wametoa elimu ufundi kwa wakufunzi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC's) ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada hizo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku saba kwa wakufunzi mafundi kutoka Kanda saba za Vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka NACTIVET Dkt. Jofrey Oleke amesema lengo la mafunzo hayo ya utengenezaji majiko sanifu ya gharama nafuu yenye kutumia kuni chache ni kuwajengea uwezo wakufunzi hao ili wanafunzi na jamii wapate mafunzo kupitia wao.
Amesema, mafunzo hayo ni sehemu ya malengo ya Serikali ya kuhakikisha watanzania wanatumia nishati safi kupitia mkakati ambao Rais Samia Suluhu Hassan ameuzindua rasmi
" Mafunzo haya yamelenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchini kampeni hii itaenea kwa kiasi kikubwa kwa kuwa vyuo hivi vinawafikia wananchi kuanzia ngazi ya chini kabisa katika maeneo ya vijiji ambapo wakipata mafunzo na kuwa na majiko hayo yanayotumia kuni chache na kwa gharama nafuu yatapunguza athari za mazingira pamoja na kukinga afya zao kutokana na athari za moshi." Amesema.
Amesema malengo ya Serikali ni kuhakikisha watanzania wanapata elimu ya kutumia nishati safi ili kupunguza athari za mazingira pamoja na afya ili kuwa na jamii salama kwa maendeleo ya Taifa na kueleza kuwa Serikali inatambua jitihada za KTO na TaTEDO na kuwataka wadau kuendelea kuunga mkono jitihada hizo ili kufikia malengo hayo ya Taifa.
Pia Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO,) Maggid Mjengwa amesema kuwa, mafunzo hayo ni sehemu ya kuchangia juhudi za Serikali katika mkakati mkubwa kabisa wa nishati safi.
Amesema, kwa KTO kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wameona umuhimu wa mkakati huo na kutoa mafunzo hayo ili kupunguza athari za matumizi ya nishati chafu na kuiomba Serikali kuendelea kushirikiana nao ili kufanikisha ajenda hiyo kupitia vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC's.)
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuendeleza Huduma za Nishati Endelevu na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO,) Estomih Sawe Amesema, mkakati wa Serikali wa kuwasaidia wananchi kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati safi na kutumia nishati safi ifikapo 2034 inahitaji ushiriki wa kila mmoja na kuwataka wadau mbalimbali kushiriki kwa kutoa elimu na Taasisi hiyo ipo tayari kutoa mafunzo kwa wajasiriamali, taasisi na wanajamii kwa ujumla.
Amesema, Katika mkakati wa kufikia asilimia 80 ya watanzania wanaotumia nishati safi ifikapo 2034 taasisi hiyo imekuwa ikihamasisha ili kufikia malengo hayo kwa kutoa elimu na kuwataka walimu waliopata mafunzo hayo kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ulembwe FDC kutoka mkoani Njombe Stanford Ndola amesema kuwa mafunzo hayo ya utengenezaji majiko sanifu na utunzaji wa mazingira yamekuwa na tija kwao, taasisi wanazofanyia kazi na jamii inayowazunguka.
" Kupitia mafunzo haya tutabeba maarifa haya na kwenda kufundisha katika taasisi zetu na jamii inayozunguka vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na tunaamini itasaidia sana katika utunzaji wa mazingira." Amesema.
Aidha amelishukuru Shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO,) kwa kuwezesha mafunzo hayo ambayo ni chachu katika vyuo vya Maendeleo ya Wananchi hususani katika utunzaji wa mazingira na uendelevu wake pamoja na Taasisi ya Huduma za Nishati Endelevu (TaTEDO,) kwa kutoa wakaufunzi mahiri walioweza kutoa maarifa ya kutengeneza majiko sanifu ya kupikia kwa kuni chache ambayo pia yatapunguza wimbi la ukataji wa miti.

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka NACTIVET Dkt. Jofrey Oleke akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo na kueleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakufunzi hao ili wanafunzi na jamii wapate mafunzo kupitia wao.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO,) Maggid Mjengwa akifuatilia wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa, mafunzo hayo ni sehemu ya kuchangia juhudi za Serikali katika mkakati mkubwa kabisa wa nishati safi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuendeleza Huduma za Nishati Endelevu na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO,) Estomih Sawe akizungumza wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa, mkakati wa Serikali wa kuwasaidia wananchi kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati safi na kutumia nishati safi ifikapo 2034.
Matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...