Kutoka kushoto  Kiongozi  wa Programu ya  Shule Bora  kutoka  ubalozi wa Uingereza  nchini Tanzania  Bi Virginia Briand akimkabidhi  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Shangwe Twamalla  baadhi ya msaada  wa vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh.Mil.140 katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Sara Mlaki akifafanua jambo

Na Khadija Kalili Michuzi Tv
PROGRAMU ya Shule Bora nchini, imetoa msaada wa vifaa vya kujifunzia wenye thamani ya zaidi ya Mil.l40 Kwa wanafunzi wa shule zilizoathirika mafuriko ya mvua za El -Nino katika Wilaya za Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani.

Programu hiyo imetoa msaada wa majiko banifu nane yenye thamani ya zaidi ya Sh.Mil. 29 Kwa lengo la kuunga mikono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira katika shule nne za msingi zilizopo Wilaya ya Mkuranga.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada hiyo, Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Sarah Mlaki, amesema msaada huo umetolewa na programu hiyo chini ya ufadhili ya nchi ya Uingereza.

Alisema msaada huo wa vifaa vya kujifunzia ni pamoja na madaftari 38,000, kalamu za wino na kalamu za risasi na kwamba umelenga kuwafikia jumla ya wanafunzi 7,300 kutoka katika Halmashauri hizo zilizoathirika ma mafuriko.

"Programu ya shule Bora imetupatia msaada huu kwa ajili ya Shule zetu zilizoathirika na mafuriko ni matumaini msaada huu utawasaidia wanafunzi wetu maana lengo la programu hii ni kuongeza ufaulu na kumaimarisha elimu nchini"amesema

Aidha amesema msaada ya majiko hayo katika Wilaya ya Mkuranga itasaidia kupunguza athari za uchafunzi wa mazingira na kwamba bado mahitaji ya majiko hayo ni makubwa katika Shule za Mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake Mratibu wa Programu ya Shule Bora ofisi ya Rais TAMISEMI, Winfrid Chiluba, amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri hizo kuhakikisha msaada huo unawafikia walengwa kwa haraka ili malengo yaweze kufikiwa.

"Naomba msaada huu uelekezwe kwenye malengo ambayo yamefanyiwa tathimini na yanajulikana wameathirika vibaya na kama vikibaki tuwaangalie wachache waliopo katika maeneo hayo..lakini pia mafuriko haya yameathiri miundombinu hivyo tunaomba programu hii itusaidie kukarabati miundombinu hiyo"amesema

Mwakilishi wa Ubalozi wa Uingereza Gertrude Mapunda, amesema mbali na msaada huo kutolewa chini ya ufadhili wa nchi hiyo, wamelenga mwakani kuongeza fedha zaidi katika sekta ya elimu Kwa serikali ya Tanzania ili kuimarisha utoaji wa Elimu Bora.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Shangwe Twamala amewashukuru Programu hiyo Kwa kutoa msaada huo na amewahakikishia kwamba msaada huo utawafikia walengwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...