*Yasema Muziki na Michezo inalipa

Shule ua Mchepuo wa Kiingereza ya Sakilight iliyopo Pugu Bombani Jijini Dar es Salaam imeipokea sera mpya ya elimu inayosisitiza watoto kujifunza kwa vitendo zaidi kwa kuanziashadarasa la somo la muziki na michezo mbalimbali.

“Tumeipokea sera hiyo nzuri na tumewekeza kwenye elimu ya muziki na michezo kwa ujumlana tuna timu za soka ya wavulana na wasichanana marufu kama Sakilight Queen na tunashirikimashindano ya vijana ya kwa upande wa soka yanayoratibiwa na Chama Cha Soka Wilaya yaIIala (IDFA),” anasema Lightness Rwegasila Mkurugenzi wa Shule hiyo.

Anasema kwamba Dunia ya sasa imebadilika na kwamba vipaji vinalipa na wao kama wadau waelimu na michezo wameua kuwekeza kwenye sanaa na michezo.

Anafafanua kuwa katika shule yake amegundua kuwa vijana wengi wana vipaji na wao jukumulao ni kuviendeleza na kuvikuza ili vijana waweze kufikia malengo yao na taifa kufaidika navipaji hivyo.

“Natoa wito kwa wazazi ambao watoto wao wana vipaji vya muziki na michezo wawaleteshuleni hapa kwani tuna mwalimu mtaalums wa Muziki ambaye atawapika vijana wetu,” anasema .

Kuhusu sera mpya ya elimu, anasema itawawesha vijana kujiajiri au kuajirika kwa haraka kwaniwatakuwa wamebobea katika fani husikal.

“Tuna mpango wa kuanzisha klabu mbalimbali za kazi za mikono kwa vijana kwa mfano upishi, ufundi Cherehani na nyinginezo kwa lengo la kuwasaidia vijana kupata ujuzi,” anasema

Anaishukuru serikali kwa kuwa karibu na shule hizo na kuzifanya zijiendeshe kwa mafanikiomakubwa.

“Naishukuru serikali kwani inatuongoza kufikia malengo yetu ya kutoa elimu kwa vijana waKitanzania,”

Kwa mawasiliano zaidi na Shule piga namba 0767847577
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...