Na Mwandishi wetu.

Shule za Green Hill za mchepuo wa Kiingereza zilizopo Pugu Kajiungeni, Ilala ,Jijini Dar esSalaam zimeipongeza serikali kwa kuweka sera nzuri ya elimu ya elimu kiasi kwamba vijanawahitimu katika viwango mbalimbali vya elimu wataweza kujiajiri.

Mkurugenzi wa Shule hizo Ndugu Kenneth Binagi anasema kwa sera ya sasa inamfanya kijanakuelewa masomo na siyo kukariri hivyo kumwezasha mhitimu kujiajiri tofauti na hapo awali.

“Hapo awali tulijita zaidi katika nadharia, sera ya sasa inatilia mkazo vitendo, ni matumainiyangu kuwa vijana wataweza kujiajiri na kuboresha maisha yao ya baadaye,” anasemaMkurugenzi huyo wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Green Hill.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, Binagi anasema kwamba sera hiyo pia imeifanya sekta ya elimu nchini kuimarika zaidi.

Kwa mfano anasema miaka ya nyuma shule nyingi za binafsi za mchepuo wa Kiingerezazililazimika kuajiari waalimu wengi kutoka nje ya nchi kutokana na uhaba wa waalimu,sasa halini tofauti, nchi ina waalimu wa kutosha na wenye ubora wa hali ya juu.

“Ninyi ni mashahidi, hivi sasa waalimu waliopo nchini ni wengi na wenye sifa,hapotunaishukuru serikali kwa kuliona hilo.

Anasema taasisi yake ina mpango wa kujenga Chuo Jijini dare s Salaam kitakachotoa mafunzombalimbali kwa vijana kama vile uuguzi na ualimu katika viwango mbalimbali vya elimu lengoni kuisiadia jamii kupata wataalam bora wa fani mbalimbali.

“Mathalani tutapata wauguzi wa kutosha ambao watatoa huduma kwa watanzania wenzetu, huondiyo mchango wetu kwa taifa letu,”

Anaotoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuwapeleka vijana wao shuleni kwake kwaniwanatoa elimu bora sanjari na miundombinu mizuri ya kujifunzia.

Mkurugenzi wa Shule za Green Hill ,Kenneth Binagi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...