NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) limeendelea kuhakikisha linawassaidia wananchi na wajasiriamali kuanzisha, kuendeleza na kuimarisha misingi ya ubunifu kwa lengo la kuongeza fursa za ajira.

Akizungumza Julai 5,2024Jijini Dar es salaam kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya kimataifa Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu SIDO, Sylvester Mpanduji amesema kupitia huduma wanazozitoa kuna wajasiriamali ambao wamefaidika kwa kupata mikopo ambayo imesawadia kuanzisha viwanda vyao.

Aidha Mpanduji amesema katika Maonesho hayo wameingia na teknolojia ya majiko ya nishati safi ya kupikia ambapo kwa watu watakaotembelea banda lao watapata nafasi ya kununua kwa ajili ya matumizi yao.

Mpanduji ameeleza kuwa changamoto ya kubangua korosho moja moja sasa suluhisho lake llimepatikana kwa kuundwa mtambo wa teknolojia ya kisasa ambao wanavikundi au mtu mmoja mmoja akitumia itasaidia kuchochea ongezeko la viwanda vidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...