Na Elizaberth Msagula Lindi,
Katika kuhakikisha rasilimali ya misitu inatunzwa na kuhifadhiwa vizuri ili iweendelevu na kuwapa manufaa wananchi hususan katika vijiji vyenye rasilimali hiyo,Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG)wamewezesha kuimarisha uhifadhi wa misitu iliyopo ukanda wa Pwani.
Uimarishaji huo umefanyika katika Vijiji 10 vilivyopo halmashauri ya Mtama ambapo misitu ya hifadhi 10 imeanzishwa yenye ukubwa wa hekta 20,732 kupitia mradi wakuongeza usimamizi shirikishi wa misitu kuanzia mwaka 2020 hadi 2023.
Miongoni mwa vijiji hivyo ni pamoja na Kijiji cha Mihima kata ya Namupa ambacho umeanzishwa msitu wa lipamba wenye ukubwa wa hekta 419 na wananchi wake wanaeleza kwamba uimarishwaji wa msitu wao kwa Kijiji umewasaidia pia katika kuwawezesha kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi unaowasaidia katika kuimarisha ulinzi wa msitu huo na kuondoa changamoto ya uvunaji holela na uvamizi na kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya msitu wa hifadhi.
Meneja wa mradi huo kutoka TFCG Yahaya Mtonda amebainisha kuwa malengo makubwa ya mradi wao ni kusaidia uhifadhi wa misitu,kuanzisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji na kuisaidia jamii kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwa kufanya shughuli mbalimbali za kuwaongezea kipato.
Amesema katika kuchochea uhifadhi mzuri wa misiti wametoa vifaa vya ulinzi kama kombati na buti kwa kamati za maliasili za vijiji ambazo wamenzisha misitu ya hifadhi ya kijiji ikiwemo Mihima vifaa ambavyo vinawasaidia kuongeza na kuimarisha usimamizi ndani ya misitu yao ya hifadhi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira katika halmashauri ya Mtama Victor Shau amesema juhudi zinazofanywa na shirika hilo kwa jamii ni mambo ambayo yamekuwa yanasisitizwa na serikali katika uhifadhi wa misitu kwani vijiji vinanufaika kwa kupata faida kutokana na uvunaji wa rasilimali hiyo na kuweza kujiimarisha kiuchumi.
Vijiji vingine kati hivyo 10 ambavyo vimeanzishwa misitu ya hifadhi ya kijiji ni Chiwerere, ChiodyaB ,Mnara, Muungano II,Ndawa,Mputwa,Mnamba na Makangara.
Home
HABARI
TFCG WASAIDIA UANZISHWAJI NA KUIMARISHA UHIFADHI WA MISITU HEKTA 20732 YA VIJIJI KATIKA VIJIJI 10 VYA HALMASHAURI YA MTAMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...