Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji, Bw. Rahim Mwanga (Kushoto), akitoa elimu kuhusu huduma na fursa zinazopatikana katika mfuko huo kwa mwananchi alietembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Afisa Mikopo kutoka Mfuko wa SELF Microfinance, Bw. Joackim Gama (Kulia), akiwaelezea baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, fursa ya mikopo inayotolewa na Mfuko huo, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Maafisa wa Wizara ya Fedha, wakimsikiliza Mkazi wa Kigamboni, Bw. Balozi Iddi (kulia), akiuliza maswali mbalimbali kuhusu elimu ya fedha, wakati alipotembelea Banda la wizara hiyo, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Boniphace Kirindimo (Kulia), akimwelezea Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini, Prof. Geraldine Rasheli,  namna ambavyo uandaaji wa bajeti ya Serikali unavyofanyika, wakati alipotembelea Banda la Wizara, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Mratibu Mkuu wa Udahili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Bw. John Adelhardus, akimweleza Mwananchi kuhusu fursa ya kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho, wakati alipotembelea Banda la wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...