Na Mwandishi Wetu - Zambia

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism) Kanda ya Afrika, Bi. Elcia Grandcourt, ambapo pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijikita katika kuendeleza ushirikiano na Shirika hilo hususan, fursa na programu mbalimbali za chombo hicho katika maeneo ya uendelezaji wa mazao ya utalii, utangazaji utalii, kuvutia uwekezaji katika miundombinu ya utalii na huduma, utoaji wa mafunzo na kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya utalii.

Kikao hicho kilimefanyika leo katika Hoteli ya Avani Victoria Falls Resort, Jijini Livingstone Zambia na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kitaalam wa UN, Bw. Jaime Mayaki, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Richie Wandwi pamoja na Afisa Utalii wa UN Tourism, Bi. Zineb Remmal.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...