Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari machache Leo Julai 06,2024 Viwanja vya Klabu ya Lugalo gofu Jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua Mashindano ya Vodacom Lugalo Open 2024.
Mkurugenzi wa Wateja wakubwa Kutoka Kampuni ya Vodacom  Nguvu Kamando akiongea machache namna Kampuni hiyo ilivyojidhatiti kudhamini mchezo wa gofu.
Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo gofu Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo akizungumza Leo Julai 06,2024 Jijini Dar es Salaam namna wachezaji zaidi ya 200 ambao wamejitokeza kushiriki Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufungwa kesho Julai 07,2024.

Na Khadija Seif, Michuzi blog 
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia , Nape Nnauye amesema amefurahishwa na muitikio mkubwa wa wachezaji wa gofu walijitokeza katika shindano 'Vodacom Lugalo Open 2924' kwa kujumuisha rika zote.


Akizungumza Leo Julai 06,2024 Viwanja vya Klabu ya Lugalo gofu Jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua shindano hilo, Nape amesema idadi ya watu wamejitokeza katika shindano hilo ni ishara tosha kuwa mchezo huo unakuwa kwa kasi nchini. 

"Pongezi kwa kampuni ya Vodacom kwa kuamia kuunga mkono jitihada za michezo hususani mchezo wa gofu kwa mara ya kwanza.

"Gofu ni mchezo uliopata umaarufu mkubwa sana katika nchi yetu, lakini duniani mchezo ambao unaweza kucheza watu wa rika zote kuanzia watoto hadi wakubwa pamoja na kuwajumuisha jinsia zote."

Nape ametoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini mchezo wa gofu hasa mashindano ya vijana ili kupatikana timu ambao itapeperusha bendera ya taifa.

"Wito kwa Makampuni mengine kujitokeza kudhamini mashindano ya vijana kwa lengo la kupata idadi kubwa ya wachezaji bora vijana katika mchezo huu."

Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo amesema kwa mara ya kwanza amechezesha idadi mkubwa tofauti na mashindano yaliyopita.

"Shindano hili ni moja ya mashindano makubwa sana ambayo yamechezwa hapa na inaonekana wadhamini hawa Vocadom wamekuja na mguu nzuri, kwa mara kwanza nimechezesha Wachezaji 200 kuanzia siku ya kwanza hadi leo siku ya ufunguzi huku kesho tunatarajia kufunga shindano hili".

Mkurugenzi wa wateja wakubwa Kutoka Vodacom, Nguvu Kamando amesema wanajivunia kuwa sehemu ya mdhamini mkuu wa shindano hilo, ambapo unaenda kuleta chachu na mapinduzi katika michezo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...