Kampuni ya bia ya Heineken Tanzania inaendelea na burudani yake ya "Afterwork by Heineken" hii ni burudani kwa wadau wake  baada ya kazi na kuweza kupumzika pamoja kwa kupata  kiywaji chao cha Heineken na burudani ya muziki. Hili ni tukio linalojumuisha watu pamoja baada ya siku ndefu ya kazi. 

 Tukio hili lenye msisimko limeanzishwa ili kukuza mtindo wa maisha unaoleta uwiano mzuri kati ya kazi na mapumziko, kwa kutoa nafasi ya kuburudika na kushirikiana na wengine. 

Ahadi ya Heineken kwa watumiaji wake nchini Tanzania  ni kuonekana wazi kwani chapa hii inaendelea kutoa uzoefu bora kwa kuthibitisha nafasi yake kama mtetezi wa usawa wa maisha na kazi. 

Kama unatafuta kupumzika au kujenga mtandao na watu wenye mawazo yanayofanana, Afterwork by Heineken ni sehemu sahihi ya kubadilishana mawazo.

 Tukio hili lilifanyika ukumbi wa Boardroom Sinza wiki iliyopita ikiwa ni  tukio lake la pili tokea kuanzishwa kwake, Tukio la kwanza lilifanyika Samaki Samaki.

Mkurugenzi Mkazi wa Bia ya Heineken Tanzania, Obabiyi Fagade akiwa na Meneja wa Masoko wa kampuni ya Bia ya Heineken Tanzania, Lilian Paschal wakati wa muendelezo wa burudani ya "Afterwork by Heineken" ikiwa ni sehemu ya kuwaweka pamoja wadau wa bia hiyo ili kupata burudani na kubadilishana mawazo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...